Tofauti kati ya "onesha" na "onyesha"

isiaka6

Member
Joined
May 9, 2013
Posts
67
Reaction score
7
Jaman wana JF naomba kujua tofauti kati ya neno "onesha" na "onyenya"
 
Hapo mkuu ipo wazi tukianza na neno ONESHA hili ni neno ambalo limetokana na neno ONA... Ikimtaka mtu aone kitu au jambo fulani kwa macho, maneno mengine ni kama onekana,oneshwa..,nk

neno ONYESHA lina tokana na neno ONYA....ikiwa na maana ya kumrekebisha mtu kitabia au kwa tendo baya alilotenda kwahiyo una muonya. Zaidi watafunguka wadau...
 
Onesha linalotumika kuonyesha uhalisia au sifa ya mto, mfano Jamaa anaonesha ni mtaalamu sana wa mavazi.

Onyesha ni neni linalotumika kufikisha ujumbe wa kuona kitu au tukio fulani, mfano Jamaa anaonyesha mitindo mbali mbali ya mavazi.

Demu anaonyesha chupi yake
Jamaa anaonesha ni mkali sana

Kifupi "Onyesha" ni muonekano wa kitu au tukio
wakati "Onesha" ni wasifu wa uhalisia fulani
 

Umeniwahi.....thanks
 

Kaka msome Hans Pol
 
Last edited by a moderator:

Hii ndio sahihi, watakaokueleza tofauti nao watakua hawajui kama wewe.
 
Jaman wana JF naomba kujua tofauti kati ya neno "onesha" na "onyenya"

Pamoja na majibu mazuri ambayo wadau wengine wameshatoa hapo juu, mjadala huu ulishawahi kuendeshwa kwa muda mrefu sana na mwisho wataalamu wa lugha ya Kiswahili walikubaliana kuwa yote mawili yanaweza kutumika kwenye muktadha wa kuona. Kikubwa ni kuwa lugha ni mali ya wazungumzaji, hivyo kwa vile wazungumzaji wanaitumia na kuilewa haina shida
 

sawa ila hebu jaribu kutuonesha mizizi ya hayo maneno mawili Onyesha na Onesha kisha uyanyumbue tupate maneno mengine kutoka kwenye hiyo mizizi, labda nitakuelewa, vinginevyo sikubaliani na wewe mkuu.
 

Havieleweki kabisa!ndio maana nahisi lugha ya kiswahili ni ya ubabaishaji mkubwa!Maneno mengine ni kama ------=Makalio,nyayo=makanyagio,meno=vitafunio! Aagh!hii lugha inachanganya tu!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 

Mkuu tafsiri na fafanuzi zako zipo sahihi kabisa, lakini nataka niongezee tafsiri nyingine hususani ni kwa neno ONYESHA.

Neno ONYESHA limenyumbuliwa kutoka katika neno ONYESHO, hivyo bado ONYESHA limebeba mantiki ya hadhira fulani ya watu kuona au kutazama maonyesho.
Hivyo neno ONYESHA lipo katika hali ya Kutendesha na kwa tafsiri ya kimombo hutumika kama exhibit au show.

Kwa msaada zaidi mnaweza kupitia kamusi ya Kiswahili ya TUKI.

on.a kt [ele] 1 see: Kusikia si ku~ hearing is not the same as seeing. 2 feel: Na~ njaa I am feeling hungry. (tde) onea; (tdk) oneka; (tdn) onana; (tds) onesha; (tdw) onwa.

ony.a kt [ele] 1 warn, admonish. 2 forbid, prevent. (tde) onyea; (tdk) onyeka; (tdn) onyana; (tds) onyesha; (tdw) onywa.

onyesh.a
kt [ele] show, exhibit,

onyesho nm ma- [li-/ya-] 1 scene (in a play).2 exhibition, show: Ma~ ya vitabu book exhibition/fair.


CC: Safari_ni_Safari bado El Toro yupo sahihi kwenye tafsiri ya neno onyesha ingawa katika neno onesha kidogo kuna mushkeli.
 
kwenye kiswahili tuna neno'' ona'' na sio '' onya'' hivyo tukija kwenye swala la mtenda au mtendewa inakuwa kama hv:-
Kutenda-ona na sio onya
Kutendwa-onwa na sio onywa
Kutendeana-onana na sio onyana
Kutendewa-onewa na sio onyewa
Kutendeka-oneka na sio onyeka
Nadhani umeelewa, ONESHA ni sahihi na sio ONYESHA.
 
Kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa mijadala ya lugha ya Kiswahili (Idhaa ya Radio One FM), kuna wakati ushwahi kuzuka mjadala wa usahihi wa ama Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba au Maonyesho ya Kimataifa ya Sabasaba...mjadala huu uliendeshwa na wataalamu wa lugha ya Kiswahili kutoka BAKITA na ulisimamiwa na Katibu Mkuu wa Baraza wa wakati huo Ndg Karekezi.

Katika mjadala huo neno sahihi lililoabainishwa kwa umma ni Maonyesho na ndilo latumika hata sasa.

Hivyo bado neno Onyesha linabeba tafsiri mbili tofauti.

onyesh.a kt [ele] show, exhibit,

ony.a kt [ele] 1 warn, admonish. 2 forbid, prevent. (tde) onyea; (tdk) onyeka; (tdn) onyana; (tds) onyesha; (tdw) onywa.

tds = tendesha
kt = kitenzi

Naomba uanagalie uzao wa maneno hayo:

Onesha (ona,ono,onwa,onekana,oneshwa)
Onyesha(onya,onyo,onywa,onyekana,onyeshwa)

The rest ni corruption ya maneno
 
Ahsanteni wakuu wote kwa majibu yenu mazuri na nimemi elewa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…