Tofauti:
sentensi changamano - ni tungo inayoundwa na kishazi tegemezi kimoja au zaidi; mfano-Mtoto aliyekuja hapa jana alikuwa rafiki yangu, Ukuta uliobomoka ulijengawa juzi.
Ilhali,
sentensi ambatano- ni tungo inayoundwa na sentnsi mbili au zaidi kwa kiungania. inaweza kuwa sentensi huru+huru,ambatano+ambatano,huru+ambatano,changamano+huru,changamano+changamano) n.k
mfano- juma analima na anna anacheza(huru+huru),mwalimu anafundisha wakai akiandika huku wanafunzi wanaandika na kumsikiliza(ambatano+ambatano), mimi ninacheza mpira ilhali wazazi wangu wanalima mara wanavuna(huru+ambatano), aliyekuja leo ameondoka lakini mimi sikumwona(changamano+huru), mti uliokatwa una kuni nyingi na walioukata walibeba kuni nyingi(changamano+changamano)