Jibu la
Behaviourist
Jibu ni rahisi sana.Horsepower ni kwa ajili ya speed wakati torque ni kwa ajili ya nguvu.
Assume kuwa wewe unapanda mlima mrefu ukiwa umebeba mzigo mkubwa begani.Hapa maana yake unahitaji nguvu nyingi.Ili uweze kumaliza kupanda mlima wako salama inabidi utembee taratibu sana(low rpm).Kwa hiyo unakuwa na nguvu nzuri ya kuupanda mlima kama utatembea taratibu(low rpm).Kama utakosea ukapanda mlima wako kwa haraka au ukiwa unakimbia(high rpm) lazima utaishiwa nguvu(torgue) haraka sana na hutafanikiwa kumaliza kupanda huo mlima.Lakini ili umalize kupanda mlima wako lazima utahitaji kutembea kutoka speed ya zero kwenda speed fulani na hapa ndipo unaona kuwa torque inaongezeka kadri rpm inavyoongezeka hapo mwanzo.
Hii maana yake ni kwamba unakuwa na nguvu nyingi(high torque) kama utapanda mlima wako taratibu(low rpm).Torque na horsepower ni ndugu ambao hawapatani.Ili uweze kukimbia bila shida(high horsepower) inabidi usiwe na mzigo mkubwa na ili uweze kubeba mzigo mkubwa(high torque) inabidi usikimbie.
The higher the rpm the high the speed(horsepower) while the low the rpm the high the torque.Kwenye graph yako hapo unaweza kuona kuwa torque inaongezeka tu hapo mwanzoni jinsi rpm inavyoongezeka lakini inapungua kadri rpm inavyozidi kuwa kubwa wakati horsepower inaongezeka kadri rpm inavyoongezeka.