Tofauti kati ya torque na Power (hp) kwenye gari

Joined
Feb 20, 2017
Posts
62
Reaction score
72
Naombeni maelekezo ya kina juu ya torque, lakini pia juu ya Power,namna zinavofanya kazi katika gari,kipi kinamtegemea mwenzie zaidi na vinamaana gani katika kuelezea uwezo wa injini katika gari husika?

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Hii ni figure ya piki piki kati ya cc 125 to 150
 
Mhhh hhh mhh.. Aisee hatari..!maelezo yako sio ya Uhakika kama jina lako..!
Umeshawahi kuiona 1vd-ftv au 1hd-fte inakosa spidi kwenye mlima sababu ya mzigo..!!?

Torque na Horsepower sio kuwa hawapatani.. Ni ndugu wa karibu sana na wanashirikiana sana tuu..!huwezi kupata Horsepower bila Torque..!
Torque ni nguvu yenyewe ya gari..
Horsepower ni spidi ya gari kutumia hiyo nguvu kufanya kazi..!

Rpms zikiongezeka sio kwamba Torque inapungua au Horsepower inaongezeka..!
Kila engine ina horsepower na Torque curves.. Kwahiyo kupanda au kushuka kunategemea na curve.. Hata Horsepower inashuka rpms zikipanda zaidi ya peak..!

Diesel engines Horsepower na Torque figures zake zinapishana sana.. Petrol engines figures zinakaribiana..!
Maana yake ukitaka gari ya kufanya kazi ngumu na kubwa chukua diesel..!
 
Hahahahaaah sio jibu langu bro, ni jibu la behaviourist nimemkopy sehemu.

Bado sikuwa na uhakika hapo bado najifunza asante kwa maelekezo yako yatasaidia nipate jibu la uhakika one day.

Asante sana ndo maana wanasema gari za mizigo na kazi ngumu mara nyingi ni diesel engine petrol ni hizi za kutembelea zaidi
 
😀😀 naomba kujua tofauti pia , huwa naona kwenye games wakati wa kununua magari
 

Attachments

  • Screenshot_20220704-095547_Bus Simulator Original.jpg
    89.2 KB · Views: 12
😀😀 naomba kujua tofauti pia , huwa naona kwenye games wakati wa kununua magari
Diesel hiyo..
HP na Torque figures zinapishana sana..!

Jitahidi utoke humo kwenye games.. Uingie road..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…