Nakubaliana na mdau hapo juu, hata hivyo niongezee kidogo kwa uelewa wangu.
Uzuri- muonekano wa mtu ambao hautegemei hali ya maisha au hadhi fulani ya maisha. Nadhani ushawahi sikia watu wakisema "Yule binti ni.mzuri sana sema tu kakosa matunzo". Uzuri kila mtu anao kwakuwa hakuna aloumbwambaya. Ila tu kivumishi "Sana" kinaweza tumika kuonesha tu kiwango cha uzuri.
Urembo- Muonekano wa binti ambao unategemea zaidi hadhi ya mtu. Hapa kiwango cha pesa na umaarufu wa mtu vinahusika. Hapa ni swala la pesa kuogezea kwenye uzuri. Inahusisha matumizi ya vipodozi, vyakula, mazoezi ya kuweka shape vizuri nk. Hapa hakutegemii uasili wa mtu bali kipato cha mtu. Kuna watu(mabinti) ambao ni warembo lakini sio wazuri.
Mvuto- hii tofauti na hizo hapo juu hutegemea zaidi watu wengine na sio muhusika. Ni namna watu wanavyoutazama uzuri na urembo wa mtu. Hata hivyo mvuto unakwenda mbali zaidi kwakuwa unahusisha vile jamii inotizama vitu kama akili,uelewa utendaji kazi wa mtu nk. Kuna watu wanamvuto wa kuwasikiliza tu yani hutamani wamalize kuongea hata kama hivo viwili hapo juu vimepungua. Mfano kwa mtizamo wangu Obama anamvuto zaidi kuliko maraisi wengi hasa katika swala la kuongea.