Ngwanakilala
JF-Expert Member
- Jun 25, 2011
- 774
- 1,464
TOFAUTI KATI YA WANAZUONI (INTELLECTUALS)NA WASOMI (INTELLECTS)
Mwanazuoni ni nani? Je, kuna tofauti kati ya mwanazuoni(intellectual) na msomi (intellect worker/intelligentsia)? Ndiyo, ipo tofauti.Wanazuoni wote, au karibu wote, ni wasomi lakini siyo wasomi wote wanakuwawanazuoni. Mara moja moja inatokea kwamba mtu ambaye hajawahi kusoma katikataasisi yeyote ya elimu huwa mpevu kifikra na kwa hiyo huwa na sifa zamwanazuoni. Lakini hii ni nadra sana. Kwa kawaida wanazuoni wengi huwa wasomi.Kwa hivyo, hatuna budi tuanze kwa kueleza wasomi ni nani. Msomi huishi kwanguvu-akili wakati mvujajasho huishi kwa nguvu-mwili. Kwa maneno mengine,mfanyakazi huishi kwa jasho lake lakini msomi huishi kwa ubongo wake.
Katikamfumo wa kibepari hii ni aina mojawapo ya mgawanyo wa kazi. Na tofauti kati yamsomi na mfanyakazi ni kubwa na ya kipekee. Inakuzwa, inatuzwa. Msomi hujivuniautaalamu na uelewa wake. Na kusema ukweli wasomi wanakubalika katika jamii kamawanataaluma ingawa utaalamu wao unaweza ukawa mkubwa juu ya jambo dogo.
Elimuya kibwanyenye huigawanya taaluma katika visehemu vidogo vidogo. Kwa hivyo, kwamfano, msomi wa uchumi siyo mtaalamu wa uchumi kwa ujumla, bali anaweza akawamtaalamu wa fedha tu au wa sarafu tu na asiwe na ufahamu wowote wa uchumi kwaujumla. Msomi wa sheria anaweza akawa mtaalamu wa masoko ya hisa tu.Anawashauri wacheza "kamari" katika soko hili - ni wakati gani mwafaka wakununua hisa na wakati gani wa kuziuza ili kujiongezea faida na utajiri.
Mfanommojawapo wa mtaalamu wa masoko ya hisa na fedha ni George Sorros, anajulikana kamamsomi aliyejitajirisha kwa kuhamishahamisha fedha kutoka soko moja kwenda sokojingine. Baada ya kutengeneza faida na kutajirika kwa njia hii sasa anafadhilimashirika yasiyo ya kiserikali ya kutetea mfumo wa demokrasia ya kiliberalikatika nchi nyingi, pamoja na Afrika. Huyu ni msomi; anachuma fedha na kuishimaisha ya anasa na ya heshima kwa kutumia akili zake "shupavu" za kucheza"kamari".
Wako wasomi wa aina nyingi tu – wakuu wa mashirika ya biashara,wahandisi, wanasheria, wanasiasa, wanaharakati, wahadhiri, watumishi wa ngaziya juu katika serikali, biashara, viwanda na wengine wengi. Lakini wengi hawasiyo wanazuoni. Wanazuoni hutofautishwa na wasomi kwa sifa kama sita hivi. Mojani kwamba mwanazuoni huchambua mambo kihistoria. Tukio au jambo limetoka wapi,liko wapi na linaelekea wapi. Mwongozo wake ni kuchambua mielekeo.Tukifananisha na mpiga picha, tunaweza kusema kwamba mwanazuoni hupiga video,sio picha. Hii haina maana kwamba kila mwanazuoni ni mwanahistoria. La hasha!Haiwezekani. Lakini kila mwanazuoni ana mwelekeo wa kihistoria katika uchambuziwake. Pili, na hili lina uhusiano wa karibu na hilo la kwanza, ni kwambaanaangalia mambo – hususan ya kijamii – katika uhusiano wake na mambo mengine.Kwa mwanazuoni, hakuna jambo lisiloingiliana na jingine. Kuweza kuelewamwingiliano ni muhimu, badala ya kulitenganisha tukio au jambo na muktadhawake.
Kwa mfano, huwezi kuelewa chanzo au vyanzo vya umaskini katika jamii bilakuelewa historia yake na uhusiano wake na utajiri. Umaskini na utajiri ni kamamapacha na vina historia moja. Matajiri wachache wananeemeka na umaskini wawengi. Kwa hivyo, kuna mwingiliano kati ya umaskini na utajiri. Hata hivyo,baadhi ya wasomi huchambua umaskini bila kuangalia historia yake na kuchukulia,bila kudadisi, kana kwamba umaskini umekuwepo tangu enzi za kale na utaendeleakuwepo milele, isipokuwa labda unaweza kupunguzwa.
Tuna mashirika mengiyanayozungumzia upunguzwaji wa umaskini (poverty alleviation) badala yautokomezaji wa umaskini. Na huwezi kutokomeza umaskini bila kuelewa vizurichanzo cha umaskini, uhusiano wake na utajiri na mfumo wenyewe unaozaa matabakaya walionacho na wasionacho.
Tatu, mwanazuoni huamini kwamba ukwelihaugawanyiki, the truth is the whole. Maana yake ni kwamba huwezi kupata ukweliwa jambo kama hujaliangalia jambo hilo katika muktadha wake. Nikitoa ule mfanomaarufu, huwezi ukasema kwamba tembo ni kama kamba nene kwa sababu umegusa mkiawake au kwamba tembo ni mpana kwa sababu umegusa sikio lake. Ili kujua ukweliwa umbo la tembo ni lazima uangalie umbo lake zima. Nitoe mfano mwingine.Ukitaka kuchambua muundo wa kiti, huwezi ukachambua miguu yake tu. Wala huwezikusema kwamba sehemu za kiti ni miguu na sehemu za kukalia na kuegemea.Ukijumlisha sehemu hizo hutapata kiti, utakachopata ni rundo la mbao! Ukitakakuelewa muundo wa kiti kizima, huna budi uchambue jinsi na katika uhusiano upi,sehemu zake zote zimeunganishwa.
Nne, mwanazuoni ni wakala wa mabadiliko yahali iliyopo, na siyo mtumwa wake. Dhamira yake ni kuigeuza na siyo kuigandishahali iliyopo. Dhamira yake ni kuleta hali bora katika jamii, hususan kwa waliowengi. Yeye daima ni mpambanaji. Anapambana dhidi ya dhuluma, uonevu,ukandamizaji na uovu mwingine popote pale ulipo. Ndiyo dhamira yake, ndiyomaisha yake, ndiyo uhai wake. Anajitambulisha na wapambanaji wenzake bilakujali wanakotoka, makabila yao, au rangi yao. Jamaa mmoja alimwandikia CheGuevara kwamba kutokana na majina yao kufanana labda wao ni ndugu wa damu. Chealimjibu kwamba yeye haoni kwamba wao ni ndugu: ‘Lakini', namnukuu, ‘kama weweunachukia uonevu popote pale ulipo, basi sisi ni ndugu, makamaradi …. bilakujali kama sisi ni ndugu wa damu'.
Tano, mwanazuoni hujali na kupiganiamaendeleo ya wanadamu, maendeleo ya wote, siyo ya wachache. Sita, ili kukidhiuelewa wa jamii na mazingira yake na ya ulimwengu, mwanazuoni hujikita kwenyeuchambuzi wa kina, uchambuzi ambao unaongozwa na nadharia iliyopevuka. Ndiyomaana wanazuoni wengi, hususan wa Afrika, wanavutiwa zaidi na nadharia yakimapinduzi ya usoshalisti. Kwa mwanazuoni huyo, ufahamu/elimu ni zana yakukosoa hali ilivyo bila kusita na kuielekeza kwenye kubadili jamii, siyobidhaa ya kuuzwa. Katika kusisitiza umuhimu wa nadharia ya kimapinduzi AmilcarCabral, mkombozi na kiongozi wa Guinea Bissau, alisema: ‘Bila nadharia yakimapinduzi hakuna mapinduzi yatakayoshinda'. Ni wazi kwamba sio kilamwanazuoni ana sifa hizo zote kama itaeleweka vizuri zaidi katika sehemuinayofuata kuhusu wanazuoni na matabaka ya kijamii. Wanazuoni wa tabakaWanazuoni ni sehemu ya jamii na wana uhusiano na jamii. Hawawezi kudai kwambawao ni wachambuzi tu wa mambo na kwamba taaluma yao haiguswi kwa namna yoyoteile na matakwa, hofu, hisia, matumaini, fikra, itikadi na mitazamo ya jamii.Kwa kuwa jamii yenyewe ya kibepari imegawanyika katika matabaka na makundi basiwanazuoni pia huwa wasemaji wa tabaka fulani au kundi fulani, ama bila kujua aubila ya kujitangaza. Tabaka linalotawala hutawala pia mawazo, fikra na itikadi,ndiyo maana katika mfumo wa kibepari itikadi ya kibwanyenye hutawala. Wanazuonina wasomi wengi hutumikia tabaka-tawala kwa njia moja au nyingine kwa kujengana kusambaza itikadi yao. Hata hivyo, wanazuoni wachache hutamani kujiunga nawanyonge na kuwatetea. Hao ndiyo wanazuoni wa kimapinduzi. Hakuna mwanazuoni aumsomi asiyejikita ama kwenye tabaka-nyonyaji au tabaka-nyonywaji. Wote hujikitakwenye tabaka fulani hata kama hawajitambui au kujitambulisha hivyo.
Na maranyingi, unaoonekana kama mgongano wa kimawazo au kinadharia ni mgongano wamtazamo uliojikita kwenye tabaka au kundi fulani. Mwanazuoni hufanya uchambuziwa kijamii ili ayaelewe vizuri mazingira kwa shabaha mahsusi ya kuboresha haliya maisha ya walio wengi. Yeye huanika uovu wote hadharani bila kujipendekeza.Katika hili uchambuzi wake unakuwa kamilifu bila kujali utamfurahisha nani nautamuudhi nani, na hata kama akisakamwa na wenye mamlaka na madaraka katikajamii, - wakiwemo watawala wa kisiasa au watawala watarajiwa au watawala wakiuchumi, - hasiti kusema ukweli kama uchambuzi wake unamuelekeza kufanya hivyo.Kwa vyovyote vile, mwanazuoni mwanamapinduzi hawezi kukosa kuchukiwa nawatawala na wenzao wa tabaka la kisiasa, political class. Kama mwanafalsafa wakimapinduzi Karl Marx alivyosema: "It is certainly not our task to build up thefuture in advance and to settle all problems for all time, but it is just ascertainly our task to criticise the existing world as ruthlessly in the sensethat we must not be afraid of our own conclusions and equally unafraid ofcoming into conflict with the prevailing powers." Kwa muhtasari, anachosemaMarx ni kwamba kwa hakika siyo kazi ya wachambuzi au wanafalsafa kutangulizakujenga mustakabali na kutatua matatizo yote kwa enzi zote, lakini ni kwahakika pia kazi yao ni kukosoa hali ya ulimwengu iliyopo wakati huo bila kusitana kutokuhofia matokeo ya uchambuzi wao hata kama haya yatawaingiza kwenyemisuguano na wenye madaraka. Niongeze kusema kwamba ni wazi kabisa kwambawanazuoni wanaotetea hali ilivyo bila shaka hawatakabiliwa na upinzani mkubwakutoka kwa wale wanaofaidika na hali hiyo.
Kwa upande mwingine, wale wanaotakakubadili hali kwa mtazamo wa wavujajasho watakuwa na hali ngumu, watasakamwa,watatungiwa uongo, watadhalilishwa na hata kujeruhiwa au kuuawa. Kwao hii siyohoja. Katika misitu ya Bolivia, wakati Che Guevara alipokutana ana kwa ana nawanajeshi mamluki wa Serikali, mmoja wao alimtambua na kulenga bastola yakekwake. Lakini alikuwa anasitasita kuifyatua. Che akamwambia, kwa sauti yautulivu; ‘Unasita nini. Fyatua risasi yako, utakuwa umemuua mtu tu!', kwa maanakwamba huwezi kuua fikra na mtazamo wa mwanamapinduzi na kweli kabisa mpaka leofikra za Che zimedumu. Katika historia yetu ya mapambano ya ukombozi tunamifano mingi ya wanazuoni waliojitolea mhanga kwa sababu ya msimamo wao kuwaupande wa umma. Patrice Lumumba alitaka nchi yake iwe na uhuru kamili ili iwezekutumia utajiri wake kwa manufaa ya, siyo Wakongomani tu, bali kwa manufaa yawatu wa Afrika kwa sababu Lumumba alikuwa muumini wa Umajumui wa Afrika(Pan-Africanism). Aliuawa kikatili na wakala wa CIA. Kwame Nkrumah wa Ghanaaliuchambua na kuukusoa mfumo wa ukandamizaji wa kibeberu, akitaka kuleta Umojawa Afrika kwa sababu aliamini kabisa kwamba wananchi wa vinchi vya Afrikawakiwa peke yao, hawataweza kumudu nguvu za kibeberu. Akapinduliwa na waliochukuamadaraka kama mwanajeshi Afrika aliyekuwa na mawazo finyu, wakamsakama nakumdhalilisha. Chris Hani, ambaye alikuwa na dhamira ya kujenga Afrika Kusinimpya kwa mtazamo wa wavujajasho, aliuawa katika kipindi nyeti cha mpito kutokaukaburu kwenda ukombozi. John Garang, kiongozi wa muda mrefu wa Sudan Kusini,alikuwa na msimamo wa kutokutenga na kuvunja nchi ya Sudan, badala yake alitakaSudan Mpya. Umma wa Sudan Kusini na Sudan Kaskazini walikuwa nyuma yake.Inasemekana alikufa katika ajali ya helikopta.
Sina hakika! Muammar Gadaffi,mwanasiasa aliyekuwa na dhamira ya kuleta mabadiliko makubwa na yenye maslahikwa nchi na jamii yake, ingawa baadaye alianza kuyumbayumba, aliuawa na majeshiya mamluki yakisaidiwa na NATO. Kosa lake? Alikuwa na mpango kabambe wa kuvunamaji yaliyopo chini ya ardhi ya jangwa la Sahara na kueneza maji hayo katikaeneo lote la Sahel. Lakini Rais wa Ufaransa, wakati ule Sarkozy, alikuwa nampango wake mbadala. Alitaka Gadaffi akubali kutoa idhini ili mashirika yaKifaransa wayavune maji hayo na kuyasafirisha kwenda Ufaransa kwa ajili yakutengeneza maji ya chupa. Gadaffi alikataa katakata. Akasukiwa mpango, nchiyake ikavamiwa na hatimaye akauawa. Leo hii nchi ya Libya imesambaratishwa nahao hao waliojiita wakombozi. Nchi na vyombo vya habari vya Magharibiwaliwakuza sana vibaraka hao na kuwatambua kama "wakombozi", ili kuhalalishamaslahi yao ambayo yalikuwa sababu kuu ya kumpindua na kumuua Gadaffi.
BY ISSA SHIVI
GAZETI LA RAIMWEMA TOLEO NAMBA 351
MAY 7, 2014