Tofauti na maana ya istilahi (TAFSIRI,KALIMANI FASILI na UKAFSIRI

Tofauti na maana ya istilahi (TAFSIRI,KALIMANI FASILI na UKAFSIRI

philosophy

Senior Member
Joined
Nov 11, 2012
Posts
104
Reaction score
42
kumekuwepo na matumizi mabaya ya maneno kama: tafsiri,kalimani,fasili na ukafsiri katika lugha ya kiswahili kwa watu wengi,hasa maneno; 'Tafsiri na Fasili'. zifuatazo ni dhana zake na matumizi sahihi:


  1. TAFSRI-Ni ni neno au istilahi itumikayo katika taaluma ya tafsiri inayotokana na kitenzi au kitendo au kitenzi jina kutafsiri ambapo maana yake ni kuhawilisha(kuahamisha) ujumbe wa kimaandishi kutoka matini ya lugha chasili hadi lugha lengawa kwa kufuata muktadha,utamaduni na isimu ya lugha husika. Mfano wa tafsiri, ni matini zilizotafsiriwa toka lugha za kigeni kuja kiswahili; kama riwaya ya 'shamba la wanyama', tamthiliya ya 'mabepari wa venisi' na bibilia ni matini tafsiri. Hivyo, unapoongelea tafsiri unamaanisha ujumbe uliohaulishwa kwa maandishi.
  2. FASILI-Ni istilahi inayotokana na kitendo cha kufasili; mantiki yake ni kutoa maana, dhana maelezo au ufafanuzi juu ya jambo fulani, kutoa maelezo ya kuhusu mana ya neno/maneno. Mfano Kamusi ni mfano mzuri wa matini ianayofasili mismiati ya kiswahili japo pia, Kamusi inatafsiri misamiati isiyo na asili ya kibantu. kwa hiyo, fasili au kufasili ni kutoa maana au dhana ya jambo/kitu fulani kinachohitaji ufafanuzi.
  3. KALIMANI-Ni taaluma ama shughuli itokanayo na kitendo cha kukalimani;shughuli hii inahusika na kuhawilisha ujumbe katika mazungumzo kutoka lugha chasili na kuupeleka lugha lengwa,kwa kuzingatia utamaduni,isimu na muktadha wa lugha na jamii husika/zinzohusika.Mfano katika siku za karibuni tunashuhudia mikutano mingi ya injili ikiwa na wahubiri wa nje wasiojua kiswahili wnaubili; lakini pia, anakuwepo mtu anayejua kiswahili anakalimani(anabadilisha maana na kuiweka ktk kiswahili).
  4. UKAFSIRI-Ni mchakato unaotoka na kitendo cha kukafsiri, maana yake ni kuhawilisha ujumbe ama wa matini andishi kwenda mazungumzo au kutoka mazungumzo na kuweka katika maandishi kutoka lugha chasili hadi lugha lengwa huku ukizingatia muktadha,isimu na utamaduni wa lugha na jamii inayohusika/zinazohusika. Mfano mzuri ni sinema au filamu ambazo kwazo wahusika wake wnakuwa wanaongea lakini maneno yanaandikwa katia runinga ama kwa kiswahili au kiingereza na lugha nyinginezo. Sinema za kitanzania ni mifano mizuri ya ukafsiri.
Matatizo ya mikanganyiko inatoke zaidi katika istilahi mbili "kufasili na kutafsiri" hakika baadha ya kusoma somo hili hutofanya tena kosa la kuchanganya dhana hizi mbili; na kila istilahi utaitumia kwa ufasaha na kulingana na muktadha wake.

ASANTENI SANA NA MUNGU AWABARIKI KTK KUIKUZA LUGHA YETU YA KISWAHILI NA KUIFANYA IWE BORA
 
Back
Top Bottom