Tofauti na sera ya kuingilia kati ya Magharibi, sera ya kutoingilia kati ya China ni chachu ya kuendeleza uhusiano wa kirafiki duniani

Tofauti na sera ya kuingilia kati ya Magharibi, sera ya kutoingilia kati ya China ni chachu ya kuendeleza uhusiano wa kirafiki duniani

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1729215385647.png


Imekuwa ni jambo la kawaida kwa nchi za Magharibi kuwa na kiherehere cha kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine hasa katika masuala ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.

Nchi hizi zimekuwa zikijifanya wababe wa kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine kwa kisingizio cha haki za binadamu. Lakini je ni kweli wanajali haki na maslahi ya wananchi wa nchi hizo ama wanajali maslahi yao binafsi?

Mara nyingi vitendo hivi vya kuingilia kati vinavyofanywa na nchi za Magharibi vimekuwa ndio chanzo cha vurugu na migogoro katika baadhi ya nchi, jambo ambalo limepelekea kuibuka kwa matabaka ndani ya jamii ikiwemo kuenea kwa chuki dhidi ya watu.

Kwa upande wa China mapema kabisa iliweka wazi msimamo wa sera yake ya kutoingilia mambo ya nchi nyingine, ikisisitiza kuwa siku zote inafuata kanuni ya kuishi pamoja kwa amani katika kushughulikia mahusiano kati ya nchi na nchi na kuunga mkono nchi kuchagua njia ya kujiendeleza kwa mujibu wa hali yake halisi.

Kama itakumbukwa ni hivi majuzi tu mwanadiplomasia anayewakilisha taifa la Marekani alisema kuwa nchi yake haitarudi nyuma kuishinikiza Tanzania kufuata kwa dhati haki na kanuni za kidemokrasia kama kipengele muhimu cha ushirikiano wake.

Kwa kauli yake hii, ina maana nchi yake inathibitisha kuwa ina haki na mamlaka ya kuingilia masuala ya ndani ya kisiasa kwa sababu ya misaada inayoipatia nchi hiyo.

Inachosahau Marekani ni kwamba kauli hii inakiuka Mkataba wa Vienna wa 1961 wa Mahusiano ya Kidiplomasia hivyo inapaswa kupingwa na kupuuzwa. Katika hotuba yake, mwanadiplomasia huyo alizungumza kwa jeuri na kiburi huku akitumia kisingizio cha misaada yao kuhalalisha sera yao kandamizi ya kuingilia mambo ya ndani ya Tanzania.

Kinyume na sera hii ya uingiliaji kati, sera ya kutoingilia kati ya China ni muhimu sana katika kujenga uhusiano wa kirafiki kati ya nchi duniani. Sera yake ya kutoingilia kati imekuwa chachu ya kuendeleza uhusiano wa kibiashara na ushirikiano kati ya mataifa, hasa kwa nchi maskini na zinazoendelea.

Baadhi ya nchi za Magharibi zinachukulia sera ya China ya kutoingilia kati kuwa haijali matakwa ya watu ya demokrasia, uhuru wa raia na kutetea haki za binadamu, hivyo sera hii inakwenda kinyume na maadili na haifai.

Lakini ukweli ni kwamba, China inaheshimu mamlaka ya nchi nyingine na inaamini kuwa kuingiliwa na nchi za kigeni ni kosa kimaadili na kunaweza kusababisha mizozo. Wahenga wanasema “Usiandikie mate wakati wino upo”, mfano mzuri ni kile kilichotokea Afrika Kaskazini na Asia Magharibi baada ya kutokea kile kinachoitwa “Arab Spring”! Kupinduliwa kwa serikali zilizoimarishwa kwa muda mrefu kutokana na kuingiliwa na mataifa ya kigeni.

Kwa upande wa Libya, kumesababisha nchi kugawanyika na kusambaratika huku ushawishi wa mashirika ya kigaidi ukiongezeka.

Uingiliaji kati wa kijeshi wa NATO kwa jina la kulinda raia umeleta mateso zaidi kwa watu wa Libya kutokana na kukosekana kwa utulivu na migogoro ya muda mrefu ya kijeshi iliyosababishwa na haohao wanaojiita walinda haki na demokrasia.

Kinyume chake, China inafuata kanuni ya kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine. Msimamo wake kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa Tanzania uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, kupitia wasemaji wake wa Wizara ya Mambo ya Nje, ni kwamba China inaamini kuwa serikali ya Tanzania na watu wake walikuwa na busara na uwezo wa kuandaa uchaguzi bila kuingiliwa na mambo ya nje na kuzitaka nchi zote kuheshimu kanuni ya kutoingilia kati, kuunga mkono uhuru wa nchi za Afrika na kulinda umoja na utulivu wao. Kwa msimamo wake, China bado inaamini kuwa serikali ya Tanzania na wananchi wake watatumia busara na uwezo huo huo kuandaa uchaguzi ujao wa serikali za mitaa bila kuingiliwa na nje.

Ikumbukwe kuwa hii sio mara ya kwanza kwa Marekani kuingilia mambo ya ndani ya Tanzania kwani Tarehe 1 Oktoba 2020, walifanya hivyo hivyo.

Nchi za Magharibi zinapaswa kuheshimu na kuiacha Tanzania na nchi nyingine za Afrika zifanye mambo yao bila shinikizo lolote kutoka nje.
 
Mbona kipindi cha magu... China ilitangaza Tanzania kwenye orodha ya nchi zisizo rafiki ...kwa Chinese investment....kama unawajua wachina vzr n bora hao wazungu hawa n kunguni kabsa ..
 
Back
Top Bottom