Tofauti ni ipi?

Yusuph Salehe

Member
Joined
Nov 12, 2010
Posts
58
Reaction score
1
Hivi kunatofauti gani kati ya SIFA na TABIA? Nisaidieni nashindwa kabisa kutofautisha!
 
sifa (nm): uzuri au ubaya wa kitu/mtu. Kwa mfano, mgombea hutakiwa kueleza sifa zake, na watu wakamhukumu kwa tabia yake
tabia (nm): mazowea (mazuri au mabaya) yanayotokana na kurudiarudia hali, mwendendo au matendo. Mfano, udaku, undumilakuwili, ukarimu, kulamba vidole wakati wa kula ni tabia.

Tafauti nyengine ni kuwa kisarufi kutokana na neno sifa tunaweza kupata tendo la kusifu, kusifika, kusifiwa lakini neno tabia haliwezi kunyambulika zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…