Tofauti ya Botswana Democratic Party na CCM!

maskini umebaki wewe tu Tanzania kwasabb ya ubabaifu na ujuaji wako eti unataka kuajiriwa kwenye kazi ya kuvaa tai na suti 🀣

wapinzani waache kutegemea ushirikiana, ramli chonganishi na kutoana kafara kwasabab ya uongozi wa ndani ya vyama vyao. waache huo utaratibu na wasisingizie wengine. Wafanye chaguzi zao za ndani kwa amani na kujali utu wa kila moja wao.

siasa za Kenya na kwingineko nadhani ni dhahiri hufuatilii, mfano mdogo tu mwezi ulopita MCA wa kenya wa county ya Wajir alichukuliwa na watu wasiojulikana hadharani mchana kweupe na kesho yake wakamkuta anaelea mtoni...


Lakini hapo Botswana hufahamu kwamba kiongozi wa chama kimoja cha upinzan aliuawa majuzi tu?

Hapo Uganda, Bob wine, Robert Gyagulanyi hakupigwa risasi ya mguu chini ya wiki 3 zilizopita?

Donald Trump hakupigwa risasi ya sikioni iliyomkosa kichwa?

Yaani mambo ya kawaida kwenye siasa yanayotokea kila pembe ya dunia unataka kuja hapa kudekadeka kana kwamba ni jambo jipya au geeni ili sijui upate huruma ya wananchi 🀣


Tanzania itaendelea kuhakikisha umoja, amani na utulivu wa waTanzania unalindwa kwa nguvu na gharama zozote zile πŸ’
 
Kwa Africa Norminal GDP Tanzania ni ya kumi (10) kwa US Bilion79. 867 Dollars wakati Botswana ni ya 27 kwa Afrika kwa GDP ya 19.699 US Bilion Dollars. Kwanini wao wapo juu kuliko Tanzania?
What is the population of Botswana VS Tanzania, by 24-10-2024, population of Botswana was 2,533,948 while Tanzania on the same data, 68,560,157

Hizo hela, (GDP), ni za mauzo ya jumla ya nchi kwa mwaka mmoja, ukizigawa kwa raia wa nchi husika ni raia wa nchi gani atapata pesa nyingi, (as an individual).

Botswana mtu mmoja atapata zaidi ya mara 7 ya mtanzania, nimekujibu tokana na mahesabu yako mwenyewe, hapo inabidi ujizomee
 
Sina uhakika kama umefanya scientific analysis, maana aliyesema Tanzania ni ya 10 na Botswana ni ya 27 sio Mimi, bali ni wataalamu zaidi yangu. I just quoted! Ahahahahaha!!

Kama wewe unajua zaidi yao, just present your argument with vivid data. Ahahahahaha!!!
 
Then the matter is closed
 

Kwa hiyo wewe unataka kusema kuanzia tupate uhuru na Botswana wapate uhuru ni chama kipi kimeleta maendeleo zaidi? CCM?

Pili hunijui hivyo usije kuongea ongea kama unanijua. Na hapa hatuongelei upinzani tunaongea malinganisho ya vyama viwili vilivyo tawala toka uhuru. Usiongelee upinzani ambao haujawahi kutawala wala Uganda ambayo sio demokrasia tunaongelea Botswana. Badala ya kujifunza na umasikini wetu wa kipato cha chini ya $2000 kwa Mwaka kwa mtu wewe unaendeleza uchawa na ndiyo sababu ya umasikini wetu
 
wewe kwa maelezo yako tu unavyojieleza inatosha kwa mTanzania yeyote kukujua ulivyo, na kwasababu hiyo nadhani unajulikana vizuri sana gentleman tena bila mbambamba yoyote 🀣

halafu nisiongelee upinzani kwasababu gani hali ya kua umerise isue ya wapinzani kupigana risasi na kuuana kishirikina wao kwa woa?

na mimi nimekueleza hilo ni jambo la kawaida sana kwenye siasa za mataifa mbalimbali duniani, na kwahivyo hakuna haja ya kulieza kana kwamba ni jambo jipyaaaa..

Hata hivyo,
CCM ndio chama mama cha tangu uhuru kinachofanya vizuri zaidi ukilinganisha na vyama vingine vikongwe barani Africa πŸ’
 
Na huu upumbavu wa sijui amani amani ndo unaifikisha hii nchi apa ilipo.tunataka maendeleo.
Utakula hiyo amani??tembeeni basi watanzania muone nchi za watu zilivyo.
Yaan Amani kwenye nchi ni zaidi ya hapo bongo.unatembea saa nane usiku na hukabwi wala kuibiwa.maendeleo ni mpaka unaona aibu.nimefika mahali nimeulizwa my nationality nikasema natoka SA mana ndo angalau kuna eleweka.Ivi kweli kwa rasilimali tulizo nazo tunashindwa kujenga barabara za juu hapo Dar??tumeshindwa kufikisha lami morogoro vijijini umatomboni uko ambako ndo mazao yanatoka???SO SAD
 
Relax bas gentleman ili ueleze uerevu vyema, makasiriko na ghadhab za nini sasa kwenye jambo muhimu kama hili?

kwamba nchi namba moja kwa uhalifu na mauji South Africa ndiyo panaeleweka?🀣

mlikutana wote wageni right? na aliekuuliza alikua anatoka ghaza, right?

Amani, umoja na utulivu wa waTanzania ndiyo inafanya tunakula, tunalala na kuamka salama. Huenda unachotamani wewe ni maandamano haramu kama yale ya chadema ya samia must go 🀣

kwahiyo unashauri waTanzania watoke kwenye amani waende Africa kusini kuuawa right?mamia ya waTz wamepoteza maisha Africa kusini gentleman. Hapafai hata kidogo.

By the way,
Tanzania chini ya serikali sikivu ya CCM chini ya kiongozi na kipenzi cha waTanzania wote Dr Samia Suluhu Hassan itaendelea kuboresha mazingira mazuri ya huduma za kijamii, siasa na uchumi ili waTanzania katika ujumla wao waendelee kufurahia matunda ya hatua muhimu kubwa mno za Maendeleo ambazo tayari zimefikiwa na zinaenda kufikiwa.

kutokuridhika ni hulka ya binadamu, unaeleweka vizuri gentleman πŸ’
 
Mimi nakuunga mkono, mimi nimefika Botswana hadi huko Kanye, kuna hospitali inamilikiwa na wasabato inaitwa Kanye Hospital nilikaa hapo kwa muda wa siku 4 nilikuwa naelekea south Africa,
 
Umenikumbusha watu wasiojulikana ambao kumbe wanajulikana ila hawatakiwi wajulikane
 

Eti kisiwa cha amani!!

 


Jamaa wameshidwa lakini kikubwa wanajali nchi na mashindano ya maendeleo sio kuiba kura. TZ hadi chaguzi za kata ni wizi. Wenzetu siasa sio kazi au biashara maana nchi ina uchumi mzuri
 

Attachments

  • af6769ed-b9f4-44c5-a77f-ece2a9e90dac.jpeg
    112.2 KB · Views: 3
  • 36556268-c7e3-4ffa-9082-ed323f7962ff.jpeg
    81.2 KB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…