Tofauti ya dini (imani) ni ushaidi wa uwepo wa Mungu

ruby garnet

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2017
Posts
2,869
Reaction score
3,852
Kuna maada mbalimbali zimeanzishwa humu kuhusu Ushaidi wa uwepo wa Mungu, Mimi leo natoa ushahidi wangu wa uwepo wa Mungu kwa kujenga hoja kutokana na Tofauti ya dini.

Swali la Musingi ni ‘kwa nini kuna dini ama imani tofautitofauti na zingine zinapingana juu ya namna ya njia sahihi ya kumuelekea MUNGU?

Wapendwa wasomaji wa bandiko hili mimi ni mkristo mkatoliki hivyo nitajibu kikatoliki swala la tofauti za dini kama ushahidi wa uwepo wa Mungu kama ifuatavyo.

Kwanza Ushaidi wa kuwepo tofauti za dini toka zama za kale

Kwa maana nyingi katika historia ya binadamu, na hata mpaka leo hii, watu wameonesha shauku kubwa ya kumtafuta Mungu kwa njia Imani na kuishi kidini (Sala, Sadaka, Ibada, Taamuli na kadhalika) hivyo mtu ni kiumbe chenye dini

  • kwa mujibu wa bibilia kuna ushaihindi wa uwepo wa dini mbalimbaili toka kitambo sana soma Kutoka 7:10-11, Yoshua 24:15, Matendo 23:6-8, Matendo17:22-25, Matendo 6:5
  • Ushaidi toka katika mazingira ya tamaduni zetu kwa waafrika hata kabla ya wakoloni au watu weupe kutuletea dini za Kikristo na Kiisilamu bila kusahau Budha, Hindu na kadhalika. Tulikuwa na dini zetu mbalimbali kwa kila jamii na tuliabudu mizimu, miti, milima dini zote hizi ziliongonzwa na hapa tunapata hoja kuu moja tu nayo ni kuwa ‘kuna kitu kilicho kikuu kuliko sisi binadamu kisichoonekana kinaongoza maisha yetu’. Jambo la ajabu dini hizi zilitofautiana kutoka jamii moja kwenda nyingine katika kuabudu ama kumuelekea Mungu

SWALI LILETALO JIBU

Ninani alimufundisha binadamu maswala ya dini?, ni namna gani Binadamu alianzisha dini? Je! Ni lini hasa?.

JIBU: Binadamu aliumbwa kwa namna ya MWILI NA ROHO, Hii ikiwa na maana Roho ni sehemu ya Mungu ama ni asili ya Mungu. Kutokana na Binadamu kuwa na asili ya Uungu amekuwa na tamaa ya kuitafuta nguvu ya asili yake. Tamaa ya kuwa na Mungu imeandikwa katika moyo wa mtu kwa sababu ameumbwa na Mungu na kwa ajili ya Mungu.

‘Ni katika Mungu tu ndipo ambapo mtu anaweza kupata ukwerli na heri ambayo hachoki kuitafuta.

HIVYO TOFAUTI YA DINI NI KIASHILIA CHA KUONESHA NAMNA TAMAA (UCHU) YA MTU ANAVYOPAMBANA KUISAKA ASILI YAKE AMBAYO NI MUNGU HATA KWA KUPAPASA.

SWALI LA NYONGEZA JE MUUNGANIKO WA MTU NA MUNGU UNATENGANISHWA (MWILI+ROHO)

Muunganiko wa Mungu na Mtu ulio haai hauwezi kutenganisha japokuwa unaweza:

  • Kusahaulika
  • Kutojulikana
  • Kukataliwa waziwazi na mtu kwa sababu mbalimbali kama
  • Uasi dhidi ya uwepo wa mabaya katika dini
  • Kutokujua, kutojali dini.
  • Mahangaiko ya dunia na mali,
  • Mifano mbaya wa waamini,
  • Maelekeo ya mawazo ya kisasa ya chuki ya dini na
  • Mwisho maelekeo ya mtu mwenye dhambi ambaye kwa hofu anajificha mbele ya Mungu na kukimbia mbali na watu wake.
  • KARIBUNI MAONYESHO YA 7 YA MADINI GEITA TUMSIKILIZE MAMA
  • NIWATAKIE MCHANA MWEMA WA JUMAPILI TULIVU
 
Kama bado binadamu anapambana kuisaka Asili yake, Utahitimishaje kusema kwamba asili ya binadamu ni Mungu?

Hii conclusion uliifikiaje?

Ulifanya Utafiti gani ukagundua kwamba asili ya Binadamu ni Mungu na si kitu kingine chochote kile?

Una uthibitisho gani kwamba asili ya Binadamu ni Mungu?

Tutahakikisha vipi kwamba asili ya binadamu ni Mungu na si kitu kingine chochote kile?

Au unafosi tu, imani zako uchwara ulizo aminishwa na kupumbazwa na dini yako, zisizo na uthibitisho wowote ule?

SWALI LA NYONGEZA JE MUUNGANIKO WA MTU NA MUNGU UNATENGANISHWA (MWILI+ROHO)

Muunganiko wa Mungu na Mtu ulio haai hauwezi kutenganisha japokuwa unaweza:

  • Kusahaulika
  • Kutojulikana
  • Kukataliwa waziwazi na mtu kwa sababu mbalimbali kama
  • Uasi dhidi ya uwepo wa mabaya katika dini
  • Kutokujua, kutojali dini.
  • Mahangaiko ya dunia na mali,
  • Mifano mbaya wa waamini,
  • Maelekeo ya mawazo ya kisasa ya chuki ya dini na
  • Mwisho maelekeo ya mtu mwenye dhambi ambaye kwa hofu anajificha mbele ya Mungu na kukimbia mbali na watu wake.
  • KARIBUNI MAONYESHO YA 7 YA MADINI GEITA TUMSIKILIZE MAMA
  • NIWATAKIE MCHANA MWEMA WA JUMAPILI TULIVU
 
Unatumia mikanganyiko kama sehemu ya uthibitisho?

Hii imenishangaza.

Hata mahakamani tumezoea kuona mikanganyiko ikitumiwa kama njia ya kubaini ushahidi wa uongo.

Lakini wewe umekuja na approach tofauti kabisa ambayo wengi hatujaitegemea.

Labda namimi nikuulize kitu..

Una amini Spiderman yupo?

Hata kama huamini nayo hiyo sio muhimu kwasababu unatambua kuwa zipo habari kumhusu.

Itakuwa vipi kama nikikupa version tofauti za mikanganyiko kwa namna ambavyo Spiderman amejadiliwa?

Je hiyo itakuwa ni uthibitisho tosha kuonesha kuwa Spiderman yupo kweli?
 
Back
Top Bottom