Kinyozi wetu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 324
- 194
Habari zenu wakuu,
Nimekuwa msomaji mzuri wa riwaya, tamthilia, mashairi na kazi nyingi za fasihi kwa kipindi kirefu sasa (sikumbuki siku sahihi niliyoanza). Nimekuwa nikifurahi zaidi kusoma kazi za fasihi zinazoakisi maisha yangu halisi (maisha ya mtanzania).
Nyingi ya kazi hizi zimeandikwa miaka ya nyuma sana, nyingi ni miaka ya tisini kurudi nyuma (nilikuwa sijatambua hili hapo mwanzo). Waandishi wengi ninaowazungumzia hapa hivi sasa ni wazee sana na wengine wameshafariki lakini mawazo yao kupitia kazi zao yanaishi kwa uhalisia hivi sasa. Waandishi hawa wengi wao hawakuwa wanazuoni na elimu ya kutisha kama waliyonayo waandishi wa kizazi hiki pia.
Nimejiuliza kwanini hawa waandishi walioishi dunia ya zamani (karne ya 20) lakini waliweza kuandika vitu ambavyo vinatokea leo? Je walikuwani watabiri? Je walikuwa manabii? Waliweza kusoma nyakati? Walikuwa na maono ya mbali zaidi ya vijana wa sasa? ama walikuwa wanaandika bila kuwa na uhakika kwa walichokuwa wakikiandika ( la hasha?). Kwa mtu anaesoma fasihi na kuielewa atakuwa kaelewa najaribu kuelezea kitu gani. Jibu nililopata kwa haraka ni kwamba walitumia muda mrefu kutafakari na kupitia kile wanachoandika ili kiisadie jamii ya kipindi kile na ijayo.
Maono, mitazamo, ushauri, hekima, busara, kauli, misemo, nasaha, tafakuri, misamiati, tafsida, , lugha ya picha na tamathali za semi imebaki ni historia kutoka kwenye kazi za hao wazee wetu. Nimepitia kazi za vijana wengi zilizoandikwa miaka ya 2000 nyingi zimekosa vitu hivyo bali zimejaa uhalisia usio endana na jamii yetu na maona yasiyo ya msingi.
Watu wamekua wakisema na kulaumu na kuuliza kwanini kazi za waandishi wa siku nyingi mpaka leo zimebaki na zinatumika katika mitaala ya shule, pasipo kujua tofauti ya uandishi (wa hao wazee wetu) na wa vijana wa sasa. Ni wakati sasa wa vijana kubadilika na kufanya kazi ya uandishi kama ajira na kuisaidia kuibadilisha jamii yao na sio kulalamika kuwa kazi zao hazinunuliwi wakati hazina mashiko na msaada kwa msomaji na kwa jamii kwa ujumla.
USHAURI: "The less we understand of what our fathers and forefathers sought, the less we understand ourselves".
Ni wakati wa vijana kukaa na kuandika vitu vinavyogusa jamii kwa kutoa ushauri, hekima, busara, nasaha na maono yanayoakisi maisha halisi, sio kukurupuka kuandika vitu visivyoisaidia jamii zaidi kuiharibu. Huwezi kuandika kazi nzuri kama hujui waliokuwa wanaandika kazi nzuri nzuri walikuwa na mtazamo gani. Kwa uhakika wa nilichoandika unaweza kupitia kazi hizi za Fasihi;
Ø ..TAKADINI
Ø ..UA LA FARAJA (THE FLOWER OF CONSOLATION)
Ø ..THE WICKED WALK; KIZAZI HIKI (W.E Mkufya, 1977)
Ø ..SIKUWA NDONDOCHA (Augustine Nnimbo, 1987)
Ø ..THE DILLEMA (W.E Mkufya 1982)
- DUNIA UWANJA WA FUJO (1975)
Nawasilisha.