Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Mbwa akiwa mlinzi kuna wanaokumbuka kumjengea kennel lakini mbwa wengine wanalala barazani au chini ya mti kwenye kivuli. Mvua ikinyesha anaachwa apambane na hali yake. Kuna wanaokumbuka kununua mifupa butcher au dagaa na kumpikia mbwa chakula. Wengine wanaachwa tu wajiokotezee, unamkuta mbwa jalalani anagombania ukoko wa ugali na kuku.
Mbwa rafiki hukaa ndani na rafiki yake, anaogeshwa mara moja kwa wiki, ana shampoo, taulo, ana chanjo za magonjwa na huonwa na vet kila baada ya miezi sita kwa check up. Mbwa huyu chakula chake ni cha makopo na kila rafiki yake akinunua chakula huangalia stock ya mbwa. Mbwa huyu anakaa kwenye makochi wanaangalia movie na rafiki zake. Mvua ikinyesha kukiwa na baridi hujisogeza kitandani na rafiki yake wakajifunika blanket.
Ukitokea na mlipuko wa kichaa cha mbwa unafikiri ni mbwa yupi atapata chanjo kati ya hawa mbwa wawili?