Kuna ngozi kungaa na kuna kujichubua. Hivyo ni vitu viwili tofauti. Kutokana na hali ya hewa, kushinda juani,upepo nk hupelekea ngozi zetu kufubaa. Ndio ile unajikuta una rangi tofauti tofauti mwilini ie ngozi ya mapaja inakuwa tofauti na ya usoni au mikononi.
Hata utumie mafuta gani ngozi yako haiwezi kung'aa kama haunywi maji ya kutosha, haupati muda wa kutosha kupumzika, una stress, huli matunda ya kutosha, huli mboga za majani, inshort huli balanced diet, unashinda juani na kwenye upepo muda mwingi,huna routine nzuri ya kutunza ngozi yako ila kubwa kuliko ukiwa hauna pesa[emoji23][emoji23]
Mafuta ni ziada tu, hivyo hapo juu ndio vya msingi zaidi.