Tofauti ya kuonesha na kuonyesha, Kuona na kutazama

Tofauti ya kuonesha na kuonyesha, Kuona na kutazama

nkamanya

Member
Joined
Sep 2, 2014
Posts
5
Reaction score
1
naomba wanajukwaa mnisaidie tofauti kati ya hayo maneno mawili Kuonesha na kuonyesha,pia kuona na kutazama
 
Tofauti ya kuona na kutazama ipo hivi; kuona jambo huendana na fikra au mawazo yako kwa wakati huo mfano macho yako yanaweza kutazama kitu bila kukiona endapo mawazo yako hayatakuwa juu ya kile unachokitazama. Pia kama uoni wako ni hafifu pia unaweza kutazama kitu bila kukiona hadi upate usaidizi wa kitu kama miwani.
Pia kama kuna kiza, ukungu nk macho yako yanaweza kutazama kitu au sehemu bila kukiona vizuri.
 
naomba wanajukwaa mnisaidie tofauti kati ya hayo maneno mawili Kuonesha na kuonyesha,pia kuona na kutazama

kuonesha inatokana na neno kuona-see
kuonyesha inatokana na neno kuonya-warn

kuona na kutazama-kutazama ni kuangalia ambapo unaweza uone au usione kutokana na sababu tofauti
 
Neno "Kuonesha"
linatokana na "Ona" likiwa na maana ya kutazama, hivyo basi tunaweza kusema, kuonesha ni kitendo cha kuweka au kutoa kitu ili watu wapate kukitazama na kukifahamu.

Neno "Kuonyesha"
linatokana na "Onya" likiwa na maana ya kukataza, hivyo basi tunaweza kusema, Kuonyesha ni kitendo cha kukataza kitu au jambo fulani, mara nyingi neno hili hutumiaka katika hali ya karipio.

Ubarikiwe,
Rev Prof: Mangalia
 
umetisha bro
 
Vizuri sana stwita kwa kuuliza swali hili, kwa kweli watu wengi wanajiuliza iwapo haya maneno ni tofauti au la.

Maneno haya mara nyingi yanatumika kwa kubadilishana kwa maana ile ile, (yaani kumwelekeza mtu aone kitu fulani). Sasa nitayachambua kama ifuatavyo:

Tukitumia kigezo cha kimofolojia, maneno haya yanaweza kuwa tofauti, hebu tuangalie mizizi au mashina ya haya maneno: ONESHA-shina lake litakuwa ONA na mzizi ON-, ONYESHA-shina lake litakuwa ONYA (Maana hapa ni nyingine kabisa) na mzizi utakuwa ONY-.

Sasa hapa nafikiri tunakwenda pamoja, umegundua tofauti ya maneno hayo kwa kufuata uchambuzi huo? Sasa kama ONA na ONYA ni mashina mawili ya maneno yenye maana tofauti basi ONYESHA na ONESHA havitakuwa na maana sawa.

Sio kweli, kwa kuangalia shina ONYA (kwa maana ya kukanya) na halafu tukalifanyia unyambuo na kuwa ONYESHA unadhani litakuwa na maana ile ile? Kuna Kiswahili hicho? Kwamba "Baba amemwonyesha mdogo wangu aache tabia mbaya". Basi kama huoni inaleta maana kutokana na shina lake, basi ujue kwamba ONYESHA na ONESHA yana maana ile ile.

Bisansaba.
 
Back
Top Bottom