naomba wanajukwaa mnisaidie tofauti kati ya hayo maneno mawili Kuonesha na kuonyesha,pia kuona na kutazama
Neno "Kuonesha"
linatokana na "Ona" likiwa na maana ya kutazama, hivyo basi tunaweza kusema, kuonesha ni kitendo cha kuweka au kutoa kitu ili watu wapate kukitazama na kukifahamu.
Neno "Kuonyesha"
linatokana na "Onya" likiwa na maana ya kukataza, hivyo basi tunaweza kusema, Kuonyesha ni kitendo cha kukataza kitu au jambo fulani, mara nyingi neno hili hutumiaka katika hali ya karipio.
Ubarikiwe,
Rev Prof: Mangalia