Tofauti ya mapokezi Korea ya Rais Samia na ya Mfalme wa Falme za Kiarabu (UAE)

Tofauti ya mapokezi Korea ya Rais Samia na ya Mfalme wa Falme za Kiarabu (UAE)

Wewe nyumbani kwako akija masikini omba omba na akija tajiri kama Mo Dewj au Bhakheresa utawapokea kwa unyenyekevu unaolingana?
Kwenye familia tu mtoto mwenye nazo anapokelewa kwa heshima kuliko aliye choka anayekuja kuomba msaada kwa wazazi.
 
Raisi Samia alipokelewa kikawaida tu wakati Mfalme wa Uarabuni ndege yake ilipoingia tu Anga la Korea ilipokelewa na ndege za kijeshi na kusindikizwa Hadi ilipotua

Maskini ana mapokezi yake na Matajiri Wana mapokezi Yao

Ona tajiri Mfalme alivyopokelewa na Matajiri wenzie wa korea

View: https://youtu.be/LQXZFgnv5M4?si=zhjuPcUvgNrDuWrw

Hakuna issue hapa. Sidhani kama thread hii ina hadhi ya kuwa hapa
 
Kiongozi naona unataka kufananisha Mbingu na Ardhi

Juzi Watanzania tuliposhindwa kuendesha Bandari zetu tuliwapa hao hao wa Dubai kuziendesha.

Halafu ndiyo utegemee Mapokezi ya Rais wetu yafanane na ya huyo wa Falme za Kiarabu 🙌
 
Nyerere pekee ndiyo alikuwa anapewa mapokezi ya kifalme kwa Malkia Uingereza Hadi Marekani kwa Reagan na Kennedy.
Ingia YouTube ujionee mwenyewe.
TENA NYERERRE ENZI HIZO AMBAZO WAZUNGU NA WAKOREA WAKIVAA KANIKI. ENZI HIZI NA YEYE ANGALIKUWA WA KAWAIDA TU
 
Raisi Samia alipokelewa kikawaida tu wakati Mfalme wa Uarabuni ndege yake ilipoingia tu Anga la Korea ilipokelewa na ndege za kijeshi na kusindikizwa Hadi ilipotua
Maskini ana mapokezi yake na Matajiri Wana mapokezi Yao

Ona tajiri Mfalme alivyopokelewa na Matajiri wenzie wa korea

View: https://youtu.be/LQXZFgnv5M4?si=zhjuPcUvgNrDuWrw

Kwani wewe hujui tofauti ya Raisi na Mfalme? Tanzania tuna raisi, hatuna mfalume wala malikia. Tanzania ni nchi ya jamhuri na si ya kifalume. Ufalume ni wa kudumu na hurithiwa kifamilia. Uraisi si wakudumu, unachaguliwa na wananchi kila baada ya kipindi kifupi na wananchi wana mamlaka ya kumuondoa wakati wo wote. Mfalme ndiye mwenye mamlaka yote kwenye falme yake, wananchi hawana mamlaka ye yote juu yake.
 
Kiongozi naona unataka kufananisha Mbingu na Ardhi

Juzi Watanzania tuliposhindwa kuendesha Bandari zetu tuliwapa hao hao wa Dubai kuziendesha.

Halafu ndiyo utegemee Mapokezi ya Rais wetu yafanane na ya huyo wa Falme za Kiarabu 🙌
Bandari kubwa hivyo, BRT si tumeangukia pua.
 
Mtu ambae kila siku kiguu na njia unadhani atapokelewa namna gani? Hata yeye angekuwa anatulia nyumbani na kutoka mara moja moja angepokelewa vizuri tu.

Nasikia kuna wakati alienda marekani akapokelewa kama mtu alomtembelea ndugu yake..unnoticed!
 
Rais Samia alipokelewa kikawaida tu wakati Mfalme wa Uarabuni ndege yake ilipoingia tu Anga la Korea ilipokelewa na ndege za kijeshi na kusindikizwa Hadi ilipotua

Maskini ana mapokezi yake na Matajiri Wana mapokezi Yao

Ona tajiri Mfalme alivyopokelewa na Matajiri wenzie wa korea

View: https://youtu.be/LQXZFgnv5M4?si=zhjuPcUvgNrDuWrw

Wewe unajaribu kulinganisha Rais ombaomba na Mfalme bilionea, anayefadhili miradi mbalimbali Ulimwenguni?😁
 
Hayo mapokezi na hata taratibu za ulinzi wa walinzi binafsi na wale wa Nchi mwenyeji, hupangwa kabisa kabla ya ziara ya Kiongozi husika kutegemea na unyeti na haswa risk zilizopo kwa mgeni.

Hata Obama alipokuja Tz wanajeshi wa Marekani walilinda Hadi Ikulu ya Tz.

Kikubwa Mama karudi na pesa ya masharti nafuu zaidi ya Shilingi Trillion 6.5
Hayo mengine tuwaachie Wenye itifaki zao.
 
Rais Samia alipokelewa kikawaida tu wakati Mfalme wa Uarabuni ndege yake ilipoingia tu Anga la Korea ilipokelewa na ndege za kijeshi na kusindikizwa Hadi ilipotua

Maskini ana mapokezi yake na Matajiri Wana mapokezi Yao

Ona tajiri Mfalme alivyopokelewa na Matajiri wenzie wa korea

View: https://youtu.be/LQXZFgnv5M4?si=zhjuPcUvgNrDuWrw

Waswahili bana tuna mambo madogo madogo badala ya kuumiza kichwa namna ya kukuza uchumi wa Nchi. Hopeless kabisaaa
 
Sasa mtu unaenda kuomba msaada halafu tena mwenyeji achome mafuta ya jet kukukaribisha kweli.? Au kwenye huo mkopo wajumlishe na gharama za kukukaribisha.?
 
TENA NYERERRE ENZI HIZO AMBAZO WAZUNGU NA WAKOREA WAKIVAA KANIKI. ENZI HIZI NA YEYE ANGALIKUWA WA KAWAIDA TU
Wewe siyo bure hiyo akili yako unahitaji msaada.
Miaka hiyo wenzio wanampeleka binadamu mwezini na Apollo..
Hiyo denial yote ni kujaribu kumshusha Nyerere viwango vya akina Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia!
Hao bado sanaaa.
Wenyewe wangekuwepo hapa wangethibitisha haya madai yangu na kukutaka uombe radhi kuwapa taji kubwa kiasi hicho.
 
Thamani ya mgeni anaijua mwenyeji. Uwezi kufanyiwa mambo mengi wakati wakijua manufaa yako kwao ni madogo.
 
Back
Top Bottom