Tofauti ya matumizi ya social media kati ya wazungu na watanzania

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
TOFAUTI YA UCHANGIAJI WA MADA KTK FACEBOOK, KATI YA MAREKANI NA BONGO:

Hello, Naitwa Sandra, Nipo New York, nampenda mume wangu Sana, naweza kufanya chochote ili nimridhishe na kumfurahisha.. Lakini hivi karibuni, nimetokea kumpenda binamu wa mume wangu.. Tena mapenzi mazito.. Naombeni ushauri nifanyeje?

WACHANGIAJI WA KIMAREKANI:

JAMES SILVER: Nadhani unapaswa kuongea na mumeo, kwa sababu ndoa ni kushea kila jambo.

SARAH WATER: OH my dear, sorry.. Imewahi kunitokea hiyo hali na mie. Ilinilazimu nijifunge kibwebwe kuiepuka ili kulinda ndoa.

MICHAEL MOORE: Ondosha fikra zako kwa huyo binamu wa mumeo.. Mfanye mumeo yale unayoyaona kwa huyo binamu yake..

MADA HIYO HIYO KWENYE JAMII FORUM, BONGO INAKUWA HIVI:
Hello, ( Jina siri yangu), Naishi Unga Limited, Arusha. Nimeolewa na Nina mtoto mmoja. Nimetokea kumpenda binamu wa mume wangu.. Nifanyeje, naombeni ushauri..

WACHANGIAJI WA KIBONGO, MAJIBU YAO:

EVARIST MASSAWE: Huna akili mpumbavu wee. Tumbili mkubwa, nyau wa kike.. YAANI unataka uanze balaa kwa binamu wa mumeo?

JOYCE MPIGAUZI: Unatutia aibu na kutudhalilisha wanawake wenzako loooh
Na vile Unga Limited ilivyo ndogo, tutakujua tu.

SELE MPEMBA:
Hivi Simba wanakipiga lini na TP Mazembe?

ANDENDEKISYE MWAKIFUGE: Kama ukiona binamu wa mumeo anazingua, mie nipo available 0710808312. Nipo Mwanjelwa.

JONES RUTTA:
Sio kosa lako. Ni kosa la wazazi wako.. Hawakutumia akili wakati wa kukuzaa.

TZ SWAG:
Wazee Nani Ana chaja ya smartphone? Simu yangu imeisha chaji.

RAMESH MATUKUTUKU: Je, una tatizo la kuwahi kileleni, upungufu wa nguvu za kiume? Inbox me na tatzo lako litaisha ndani ya wiki moja ujenge heshima

ANDREW THE DON:
Wow.. Mtoto uko Bomba.. Ni add please..

MTUMISHI: Wewe ni kahaba uliyeshindikana, unatakiwa Uokoke.. Njoo ufanyiwe maombi.

MAC MUGA: Tengeneza mpaka milioni mbili ndani ya wiki moja tu bila kuathiri kazi zako. Kwa maelezo zaidi nitafute 07356

MWAJEY MIKIDADI: Pumbaaaaaf.

DEVOTA JILANGILA:
Napita tuuu.

DULLA BOY:
Mie huwa sichangiaji post za kijinga kama hii...

C&p
 
Ila wale Wanao comment kwenye ukurasa wa EATV nafikiri wengi ni under 25, maana akili zao za kitoto sana, halafu mambo mengi yanayoendelea duniani hawayajui kabisa
Ndiyo maana mada za udaku zina likes na comments nyingi za kishamba .

Ila mada za msingi zinaishia kupuuzwa shida ni elimu elimu elimu .

Tuache kujibu kwa mihemko
 
Dah yaan nimecheka aseee jpili ya leo si ya mchezo kwa hii kitu imeniletea good mood kutoka kwenye bad mood....[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mzungu muache alivyo sisi tunatoana stress na tunapeana upendo kwenye social media wange iga kwetu wasingekuwa na stress wala kukaa kwenye nyumba za wazee
 
Hahahahaha nadhani kwa Africa wanaigeria wanaongoza yaani mpaka hua wanatimuliwa kwenye forums/groups zingine,
wapo negative minded sana, wana mihemko, wanajifanya wanamjua sana Yesu, wanaweza wakamsimanga mtu mpaka akazimia.
 
Bado "sisi tusio na wake tunakoment wap?"
 
Nilichogundua, ni kwamba sehemu unayoishi akili huchukua tabia za eneo hilo..

Mfano mdogo, angalia wanaoishi manzese, wanoishi magomeni, wanaoishi masaki, wanaoishi mbeya, wanaoishi mwananyamala, wanaoishi kongwa, waoishi namtumbo, n.k, n.k

Ukilinganisha aina zao za fikra utapata jibu..[emoji41][emoji41]
 
Hao wamarekani wanavyochangia ndiyo vile watu wa Dar wanavyochangia mada...

Hao wakibongo wanavyochangia ndiyo vile watu wa miakoni nje ya Dar wanavyochangia mada...

Akili za kuambiwa...



Cc: mahondaw
 
Mzungu muache alivyo sisi tunatoana stress na tunapeana upendo kwenye social media wange iga kwetu wasingekuwa na stress wala kukaa kwenye nyumba za wazee
Nasikia Forbes wametuweka top 3 ya stressed countries tunachuana na Uingereza na Amerika
 
Hahahahaha nadhani kwa Africa wanaigeria wanaongoza yaani mpaka hua wanatimuliwa kwenye forums/groups zingine,
wapo negative minded sana, wana mihemko, wanajifanya wanamjua sana Yesu, wanaweza wakamsimanga mtu mpaka akazimia.
Huwa natafuta forums za kuwapata sijazijua bado zaidi ya BBC focus on Africa anakotangaza mnaija mwenzao Okwoche
 
Ukiwa inferior na hutaki kukubaliana unazidi kudidimia...ukijigundua ni inferior inakupa nafasi ya kujirekebisha...penye udhaifu tujiseme,tukificha tunakuwa wanafiki kwa nafsi zetu wenyewe...ukweli ni kwamba wengi wetu bado hatujawa na ustaarabu wa kutumia mitandao ya kijamii...mfano ni humu humu JF mtu analeta sledi anaomba ushauri watu wanaanza kupiga stori tafauti na mada au kuchombezana au kujibu kunya...tunafaa kustaarabika eneo hilo mostly tumekosa staara!
Inferiority kill us
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…