Tofauti ya mavazi wanayovaa raia wa Rwanda, Uganda na Tanzania kwenye harusi

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304




Haya ni mavazi wanayovaa wanyarwanda kwenye harusi bila kujali kabila la mtu, harusi zote za wanyarwanda huvaa hivyo. Napenda sana mavazi yao.







Haya ni mavazi ya waganda kwenye harusi bila kujali kabila wote huvaa hivi kwenye harusi na napenda sana mavazi yao.

Sasa twende kwa Tanzania:

Tanzania ni vurugu kila mtu anajivalia vazi lake analojisikia, hakuna vazi maalumu labda kwenye kitchen party ndio watu angalau hushona sare sare lakini hakuna vazi maalumu. Wengine huvaa ata vimini kila mtu anatoka vile anajisikia.

Kwa tanzania wasimamizi peke yao ndio hushona sare, raia wengine wanakuwa huru kuvaa watakavyo tofauti na nchi za Uganda na Rwanda. Huwezi ukavaa tu vimini vyako kwenye harusi, hizo nguo uvaliwa club.

Sorry sitoweka picha za Tanzania sababu hakuna vazi maalumu la nchi. Mkiwa na vazi maalumu nitarudi kuweka picha. Samahani kwa hilo.
 
Mkuu upo sahihi kwa Tanzania,kuna siku bidada alivaa kimini hicho balaa(hajachuchumaa chupi inaonekana).Ukumbi mzima uliamishia macho kwake.
 
Msilaumu sana, sisi hatuna vazi la taifa bado.
 
Sio tu Rwanda na uganda pekee mbona warundi wanavaaga hivyo hivyo tena siotu kwenye sherehe /shughuri Bali hata makasani wanavaa jiridhishe kwa ku Fanya tafiti ya kutosha ndugu mhariri
 
Vazi la Rwanda linaitwa "Mshanana" ni maalumu kwa shughuli zozote za harusi au sherehe yeyote ya kitaifa ama kimataifa. Jamaa wako stricted kiaina maana hawana Uhuru wa kuishi wanavyotaka.

Kwa Bongo mambo ni nyooso..kila mtu anaamua kuvaa anachoona kinampendeza..mavazi ya Rwanda kuna wengine wakivaa wanakuwa kama Wacambodia au wavetnam jinsi yanavyowachoresha.
 
Kwani kuna ulazima kwenye harusi wote tuvae sare??
 
Nabaki na Tanzania yangu kama tulivyo makabila tofauti na tunaishi kwa upendo basi na kwenye tafrija nyingi tunatokea tofauti tunafurahia tofauti zetu na tunaijenga nchi yetu nyie wapuuzi mnaokuja kuomba pa kulala ndio mnaokuja na kelele kama hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…