MZAZI MASKINI;
Kazana kusoma mwanangu ufaulu vizuri mitihani yako ili baadaye uje kupata kazi nzuri utukomboe na umaskini huu.
MZAZI TAJIRI;
Kazana kusoma ili baadaye uweze kutafuta na kusimamia pesa zako vizuri bila kuibiwa na waliosoma.
MWISHO;
Maskini wataendelea kuwa maskini tu,maana siku hizi hata kama una elimu ya juu na ufaulu mzuri kazi hakuna...
Matajiri wananunua hizo nafasi za kazi na kuwapatia watoto wao ambao wana spirit ya kutafuta na kusimamia pesa mwisho wa siku ufisadi kila kona...
Wazazi maskini badilisheni mitazamo yenu,wajengeni watoto wenu katika kujua kutafuta na kusimamia pesa..
Asanteni
Nimeipenda hiyo point ya matajiri kununua nafasi za kazi. Kuna ukweli kwa kiasi fulani. Lakini nilitegemea elimu imkomboe mtu kifikra kwamba asione kwamba mwisho wa elimu yake ni kuajiriwa! Kuna ukweli kabisa vijana wetu wanaoandaliwa vyuoni sasa, mitazamo yao ni juu ya ajira au ugumu wa kupata ajira, ndicho kilichopo vichwani mwao na hii inazuia fikra zao kuona avenues nyingine hata kabla ya kumaliza shule. Nadhani sisi wazazi tunapaswa kujitengenezea mtaala mwingine wa namna ya kumlea mtoto wa sasa ili aweze kupambana na ulimwengu wake i.e. asiwe tegemezi wa system. na hapa tunahitaji kuwajengea watoto wetu aggressiveness spirit ili anapomaliza chuo asijikunyate na mawazo ya ajira. Along side inabidi wazazi unapomsomesha mtoto uwe unamuwekea kama akiba fulani ili kumwezesha ku take off akishamaliza chuo kuliko anamaliza afu mnabaki mnatazamana. kwa sasa mitaala ya vyuoni haiwaoneshi namna ambavyo wanaweza kutoka katika fikra tegemezi.
baada ya kusoma hicho kitabu cha rich dad mmefaidika vipi? je mliyosoma mnayaweka kwenye matendo au yameishia pale kama mnavyosoma magazeti ya shigongo?
hayo unayoyauliza tulisha ulizwa zamani sana.sasa hivi tupo kwenye vitendo.mimi sijaajiriwa,naishi kwa nguvu zangu kitaa japo nipo chuo.na nipo kwenye mchakato.wewe kama huna mood na vitabu acha tu .alafu usifikili kila mtu yupo kinadhaliabaada ya kusoma hicho kitabu cha rich dad mmefaidika vipi? je mliyosoma mnayaweka kwenye matendo au yameishia pale kama mnavyosoma magazeti ya shigongo?