Tofauti ya neno "ndio" na "ndiyo"

Kwa kadiri ya uelewa wangu katika lugha ya kiswahili(soit ma deuxième langue) tofauti baina ya maneno hayo mawili ni:

~NDIO ni kivumishi kioneshi (V).kivumishi ni neno linaloelezea zaidi nomino au kiwakilishi.Neno hili, NDIO, linaweka mkazo katika KUONESHA nomino/kiwakilishi.
Mfano;Hii NDIO nyumba iliyojengwa.

~NDIYO ni neno lenye maana ya KUKUBALI jambo au kitu.
Ni kinyume cha HAPANA.
Mifano;
-Je,una watoto?NDIYO

-Je,hii ndio nyumba iliyojengwa nawe?NDIYO
 
Ibn ingia kwenye kamusi vizuri. Ndiyo ina maana mbili ya kukubali na kuonyesha nomino. Wingi wa ndiyo tunapata ndio. Huwezi sema hii ndio miti yangu. Utasema hii ndiyo miti yangu. Huu ndio mti wangu. Hii ndiyo nyumba yangu/hizi ndizo nyumba zangu.
 
I think this explanation makes more sense than the rest.

Hii ndio ndiyo yenyewe
 
Kwahiyo ndio na Ndiyo , ndiyo nini sasa????😅😅
 
Neno sahihi hapo ni ndiyo hilo ndio limekuja ka hivi sasa yanavyokuja maneno alafu badala ya halafu, hangalia badala ya angalia, araka badala ya haraka nk
 
safi
 
Ibn ingia kwenye kamusi vizuri. Ndiyo ina maana mbili ya kukubali na kuonyesha nomino. Wingi wa ndiyo tunapata ndio. Huwezi sema hii ndio miti yangu. Utasema hii ndiyo miti yangu. Huu ndio mti wangu. Hii ndiyo nyumba yangu/hizi ndizo nyumba zangu.
Umeanza vizuri halafu ukajichanganya.. maelezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…