Moderators nashukuru kwa kuuleta huku huu uzi, wataalam wa hivi vyombo vya usafiri JF RugambwaYT mng'ato RRONDO Jimmie Gatsby MANI Mshana Jr na wengineo msaada wenu tafadhali.
mkuu habari.... niende kwenye mada moja kwa moja
suzuki escudo , suzuki vitara, suzuki grand vitara hiyo ni gari moja hayo majina yasikuchanganye
first generation ilitoka 1988 ikiitwa
suzuki escudo kwa soko la japan Japanese domestic market (JDM) na baadhi ya masoko machache kama asia spec na south america spec
ila kwa soko la US na EUROPE hii gari ilienda kwa jina la suzuki vitara
ilipofika second generation na kuendelea (now wapo forth) jina la
suzuki grand vitara likazaliwa
ila ikabaki vilevile kwa soko la japan ikaendelea kuitwa
suzuki escudo ila kwa US spec na UK spec ikaitwa
suzuki grand vitara
kwahyo mkuu usihofu ukiona inaitwa
escudo basi jua hyo ilitengenezwa kwa ajili ya soko la japan (JDM) then ukiona inaitwa
grand vitara basi jua hyo ilitengenezwa kwa ajili ya soko la US na UK
ni kama tu
toyota corola X assista ukiinunua ya asia spec itaitwa
toyota altis
na ndio maana unaona hata kuna vitu ndani pamoja na uimara zinaweza tofauti kwa sababu kila moja hapo ilitengenezwa maalumu kwa ajili ya soko fulani kutokana na vigezo husika pamoja na mazingira
ushauri ukitaka kuchukua ifate inayoitwa escudo sababu hii ni japanese domestic market (JDM) na mazingira yetu tanzania gari zinazoweza kuhimili shida zetu ni hizo JDM
Nina imani maelezo yangu yatakuwa yamekusaidia kidogo