"Tobo" linaasili moja na neno "toboa"
Maneno mengi yenye asili moja na "tobo" ni "tobwe", "kitobwe", " kitobo",
Yote hayo yanamaanisha tundu haijalishi kama kubwa au ndogo
Nb: tobwe wakati mwengine hutumika kumaanisha "mtu mjinga au mpumbavu"
"tundu" nayo ina maana ile ile kama "tobo", haijalishi kubwa au ndogo
Nb, neno "tundu" halina asili moja na neno "tundua"
Kwa matumizi ya kila siku watu wengi huita tobo ikiwa tundu ni kubwa na imekosa shape au uwiano,