Tofauti ya uchangiaji wa mada ktk facebook, kati ya Marekani na bongo

Tofauti ya uchangiaji wa mada ktk facebook, kati ya Marekani na bongo

Kajole

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2011
Posts
1,668
Reaction score
1,643
TOFAUTI YA UCHANGIAJI WA MADA KTK FACEBOOK, KATI YA MAREKANI NA BONGO:

Hello, Naitwa Sandra, Nipo New York, nampenda mume wangu Sana, naweza kufanya chochote ili nimridhishe na kumfurahisha.. Lakini hivi karibuni, nimetokea kumpenda binamu wa mume wangu.. Tena mapenzi mazito.. Naombeni ushauri nifanyeje?

WACHANGIAJI WA KIMAREKANI:

JAMES SILVER: Nadhani unapaswa kuongea na mumeo, kwa sababu ndoa ni kushea kila jambo.

SARAH WATER: OH my dear, sorry.. Imewahi kunitokea hiyo hali na mie. Ilinilazimu nijifunge kibwebwe kuiepuka ili kulinda ndoa.

MICHAEL MOORE: Ondosha fikra zako kwa huyo binamu wa mumeo.. Mfanye mumeo yale unayoyaona kwa huyo binamu yake..

MADA HIYO HIYO KWENYE JAMII FORUM, BONGO INAKUWA HIVI:
Hello, ( Jina siri yangu), Naishi Unga Limited, Arusha. Nimeolewa na Nina mtoto mmoja. Nimetokea kumpenda binamu wa mume wangu.. Nifanyeje, naombeni ushauri..

WACHANGIAJI WA KIBONGO, MAJIBU YAO:

EVARIST MASSAWE: Huna akili mpumbavu wee. Tumbili mkubwa, nyau wa kike.. YAANI unataka uanze balaa kwa binamu wa mumeo?

JOYCE MPIGAUZI: Unatutia aibu na kutudhalilisha wanawake wenzako loooh
Na vile Unga Limited ilivyo ndogo, tutakujua tu.

SELE MPEMBA:
Hivi Simba wanakipiga lini na TP Mazembe?

ANDENDEKISYE MWAKIFUGE: Kama ukiona binamu wa mumeo anazingua, mie nipo available. Nipo Mwanjelwa.

JONES RUTTA:
Sio kosa lako. Ni kosa la wazazi wako.. Hawakutumia akili wakati wa kukuzaa.

TZ SWAG:
Wazee Nani Ana chaja ya smartphone? Simu yangu imeisha chaji.

ANDREW THE DON:
Wow.. Mtoto uko Bomba.. Ni add please..
MTUMISHI:

Wewe ni kahaba uliyeshindikana, unatakiwa Uokoke.. Njoo ufanyiwe maombi.

MWAJEY MIKIDADI: Pumbaaaaaf.

DEVOTA JILANGILA:
Napita tuuu.

DULLA BOY:
Mie huwa sichangiaji post za kijinga kama hii...
 
Hawa mademu wanao cheza na twiga star mbona siwaelewi, kuna demu ana jezi namba 7 yaani kama men vile

MGC
 
😀 mkuu naona wabongo wana majibu mubashara No unafki wanakuchana hapo hapo
 
Nisingeona koment ya jamaa anaulizia mechi ya Simba na TP Mazembe nisingekubali kwamba hizo ni koment za JF
 
Mbona hakuna cha kuchekesha hapo zaidi naona akili duni za wabongo na mitusi tu!

Ndio aina ya wachangiaji tulionao humu!! Mtu anataka ushauri au ameleta bandiko lenye kuhitaji weledi lakini unashangaa kukuta majibu ya kitoto tupu!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
😂😂 evarist massawe ana nini lakini mbona povu hivo.
 
jamii forum iliingiliwa na watoto! dawa ni moderators kufanya kazi yao! au waweke kipengele cha anaekuwa mwenye mada awe na access ya kucontrol/ kudelete/hide comments za ajabu
 
Back
Top Bottom