Tohara kwa Wanawake ina faida gani?

Hakuna faida yeyote kukeketa wanawake bali ni hasara tupu. Ni moja ya mila potofu na ya kijinga sana tu
 
 
Haina faida, inachofanya ni kumnyima mwanamke haki yake ya kufurahia tendo la ndoa.

Tohara haipunguzi umalaya, kama mwanamke ni malaya, atafanya umalaya hata kama ametahiriwa.
 
Hebu ifanywe tadhimini sasa ya kuwa ni madhara kiasi gani yaliyopo kwa wanawake waliotahiriwa na wasiotahiriwa na ni asilimia ngapi kwa sasa.
 
 

Hayo uliyotaja yote si ya kweli bali unyanyasaji wa hali ya juu. Kama kweli kuna faida basi waachwe wenyewe wajipeleke hospitali kwa hiari kuomba hiyo huduma, mbona wanalazimishwa??

Kuna mengi tu siku hizi tunayasikia kama breast enlarment, face uplifts, kutoa tumbo n.k ambayo wahitaji wenye uwezo wao wanaenda hospitali wanalipa na wanafanyiwa. Whether yana faida kwao ama la, hakuna wa kuwauliza maana wamechagua kwa hiari yao bila kushurutishwa. Mbona kwenye ukeketaji hatuwapi uhuru huo kama kweli kuna faida za wazi nyingi hivyo??

Watu wanaoendekeza zaidi hili zoezi ni wale walioko vijijini kule ndani ndani. Huku mijini sehemu ambako watu wanajua madhara yake wanalipiga vita. Ni kwa nini? Kwamba kweli kuna kitu kizuri ambacho walioelimika hawajakigundua kiasi hicho? Hapana! Huu ni utamaduni wa kishenzi tunaohitaji kuondokana nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…