Toka ahamie Kinondoni amebadilika sana

Toka ahamie Kinondoni amebadilika sana

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Huyu jamaa nlisoma naye chuo miaka ya nyuma. Ni msukuma wa Mwanza. Alikuwa jamaa fulani hivi wa Mkoani amegangamaa.

Baada ya hapo ktk harakati za maisha akahamia Kinondoni. Jamaa amebadilika sana. Amekuwa na kitambi, nyoronyoro sana. Siku nimeenda kumtembelea tumetoka enda kula tunarudi akaanza nizungusha maduka ya urembo kuna lotion anatafuta.

Mara tumeipata anauliza cream fulani ya kupaka usoni. Sikumwelewa kabisa. Nikaanza ku recall siku ile mchana tulienda kula alikula chips na sausages na jioni alikuwa chips kuku bwege.

Kiasi tu then akanywa na beer chupa mbili. Nilishangaa sana naye alinishangaa nakula mchemsho wa samaki mkubwa na chapati nne usiku na wakati mchana nlikula ugali na mbuzi choma akashangaa huo ulaji anasema si mzuri.

Kifupi jamaa kabadilika sana imagine mtu kamaliza chuo mwaka 2005 mpaka leo hajaoa. Ila anawafaham na kufahamiana na wasanii wengi kinyama... jamaa alinichosha zaidi aliponambia huwa wanapiga maji na TID daaah nikaona mwana ndio amepotea kabisa.

Jamaa ndio tumempotezea kinondoni. Yupo tu hata mademu anapiga nao stories kinyama wakati sisi wengines stories ni chache sana vitendo vingi. Kila sehemu wanamwita Muddy Zungu... Madada wa salun mpaka wanamshika makalio anacheka tu

Huko nyuma hakuwa hivi kabisa.
 
Back
Top Bottom