Tongoza Vs Shawishi -- Which is which ?

Tongoza Vs Shawishi -- Which is which ?

Judgement

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2011
Posts
10,326
Reaction score
4,785
Akichangia hoja ya Waziri wa Elimu , hivi majuzi Mhe. Tundu Lissu, namnukuu ;

"Huu muswaada aliouleta waziri hauna mantiki wala tija yeyote ktk Elimu ya Tanzania. Hii ni sawa serikali iliopo madarakani kutaka kutumia huu ubabaishaji KUTONGOZEA kura za 2015"
(mwisho nukuzi)

Ndipo aliposimama Mnadhimu wa Sirkali akija kwa ticket ya "kuhusu utaratibu aidha muongozo wa spika"

Mhe, Lukuvi alilenga kwenye neno TONGOZA kwamba linashabihi ktk lugha za kuudhi, aidha si ktk lugha nzr za kibunge.
Alimtuhumu Mnadhimu mwenzake wa upande wa pili.

Palisimama wabunge takriban wawili upande wa upinzani , nakumbuka Mhe. Machali na Mkosamali wakimtete Lissu kwa maana ya kua lugha ile haikua ya kuudhi.

Aidha upande wa gavmenti walisima wa hesh, wawili wakimsapoti Lukuvi.

Mhe, Ole Medeye alidai yeye ni lekchara wa Kisw na anathibitisha lugha husika ni ya kuudhi.

Kabla hajaongea Medeye , ktk ufafanuzi wake Machali alisema neno TONGOZA halina tofauti na SHAWISHI.

Akaja Mhe, Ole Sendeka yeye alimuunga mkono Lukuvi , na akamithilisha kwa kusema: "Kama TONGOZA ni SHAWISHI, je? Kuna mtu anaweza KUMTONGOZA mamaake ?"

Nna imani baadhi yetu hapa watakua waliuona mjadala huu, na wale ambao hawakuuona basi ndiyo watanufaika kuelewea hapa.
Nami nafsi ikajikuta imeshindwa kuliacha hili lipite ilhali na sie tujiitao "wafikiriaji wakubwa" hatujalijadili .

Nihitimishe kwa kusema ubishi huu ulitukia ukimkuta Naibu spika, ambae ktk maamuzi yake juu ya hili hakuweka bayana kati ya Lukuvi na Lissu nani mshindi.
 
Probably it's not bad if we glanced to our neighbours about the matter! Tukubali/tusikubali ndiyo ukweli utabaki kua hivyo, kua Kingereza na Kiarabu viko more advance than Kiswahili.
SEDUCE => to act as suggested having sexual intercourse. (hawana maana ya ziada tofauti na hiyo)
SHAWISHI => Convince , Persuade, to act as suggested, (hawanasibishi convince inatumika katika ku'request Penzi). Kimaono yangu kama kwa jirani zetu maneno haya hayafanyi kwa kufanana, kwetu sie iweje tuyafananishe?
 
Tongoza = kumrai au kumshawishi mtu ili akubali kufanya mapenzi nawe , mwambie kaka yako kuwa utamtongoza mkewe , tizama kama patakalika hapo !!!!

Shawishi = kumrai mtu ili akubali ulisemalo bila ya kuhusiana na ngono. Mwambie kaka yako kuwa utamshawishi mkewe , anaweza hata kukusaidia kumshawishi.
 
Huwezi kutumia neno "Tongoza" zaidi ya kumlahai mwanamke kimapenzi
Kama vile huwezi kutumia neno "Simika" zaidi ya kusimama kwa sehemu yako za siri
Kwa wale ambao kiswahili ni "mother tounge" tukisikia maneno haya yanatumiwa vyengine tunashangaa sana 😉
 
Back
Top Bottom