Toni Kabetha katika ubora wake; Hebu pitia nondo zake 10 ziko hapa

Toni Kabetha katika ubora wake; Hebu pitia nondo zake 10 ziko hapa

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Ni masiliamali na mtanzania ndugu Tony kabetha ameongea mambo mengi sana mazito kuhusu sekta mbalimbali ingawa mimi nimevitiwa sana na hoja zake zilizohusu kilimo cha Tanzania.

Nikatamani sana ndugu Bashe angekaa amsikilize kwa vituo, huenda hoja zake zikalisaidia taifa.

Hizi hapa baadhi ya hoja zake

1. Serikali iwatafutie wananchi masoko ya uhakika ya mazao yao. Kukiwa na masoko ya uhakika ya mazao mashamba watayatwfuta wenyewe wakisukumwa na soko.

2. BBT isichukue watu ambao hawajihusishi na kilimo. Serikali iwawezeshe vijana katika mazingira yao.

3. Serikali ichukue mkopo maalum kwa ajili ya kuwakopesha wakulima ambao utakopeshwa kwa kukatwa service charge tu. Tofauti na ilivyo sasa.

4. Serikali iwekeze zaidi kwenye elimu inayohusu kilimo ambapo watafundisha wananchi kuhusu masoko na namna ya kuyafanya mazao yao yauzike kimataifa.

5. Serikali ibadili utaratibu ili maonyesho ya kilimo yalete mataifa na makampuni yanayohitaji bidhaa zetu.

6. Maonyesho ya kilimo yafanyike kila mwezi na kila eneo litangaze zao lao ambapo serikali kupitia balozi zake wawalete walaji ili kuwakutanisha na wakulima.

7. Serikali iwaunganishe wakulima ili wawe na uwezo wa kukidhi mahitaji ya soko kwa kuzalisha kwa wingi.

8. Serikali inatoa ruzuku kidogo sana lakini mara zote hizo pembejeo huja kwa kuchelewa sana kwa hiyo hazitusaidii wakulima.

9. Serikali ipunguze mazao ya kipaumbele ili iyahudumie kwa uhakika.

10. Serikali iachane na utaratibu wa kuwaambia wakulima soko liko mahali Fulani badala yake iwe dalaja la soko.

Haya ni baadhi tu ya mambo aliyoongea alipokuwa akihojiwa na chief odemba wa star tv.
 
Back
Top Bottom