Tony Elumelu Foundation (TEF Connect) imefungua dirisha la usajili kwa wajasiriamali

Tony Elumelu Foundation (TEF Connect) imefungua dirisha la usajili kwa wajasiriamali

Samedi Amba

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2018
Posts
227
Reaction score
178
Habari za muda wadau na wanajamvi,

Tony Elumelu ni mwana wa afrika, mjasiriamali, mpambanaji na mkarimu pia. Alianzisha foundation ya Tony Elumelu, mnamo mwaka 2010. Nia ilikuwa ni
kuwawezesha wanaume na wanawake katika bara letu (la Afrika), kutia chachu ukuaji wa kiuchumi, kuondoa umaskini na kutengeneza fursa za ajira. Tunaamini kuwa sekta binafsi ina sehemu nyeti katika kuzalisha mali na rasilmali watu.

tef-signup.PNG


Mnamo mwaka 2015, mlango ulifunguliwa kwa ajili ya kuwafadhili wajasiriamali barani Afrika, kupitia kampuni ya Tony yenye jina "Heirs Holdings". Aliunda programu maalum yenye jina "The Tony Elumelu Foundation (TEF)". Aliwekeza dau la $100,000,000 (dola milioni mia moja za kimarekani) kwa ajili ya kuwafadhili wajasiriamali 10,000 ndani ya muda wa miaka kumi.

TEF imewezeshwa na kutiwa shime na mashirika kama vile United Nations Development Program (UNDP), the African Development Bank na United Bank of Afrika.

Kila mwaka (tangu 2015), kila mshindi hupewa $5000 (dola elfu tano za kimarekani, au milioni Kumi za kitanzania), kwa ajili ya kuanza au kukuza biashara.

Ikumbukwe kuwa sio lazima uwe na biashara inayotembea tayari. Hata idea tu inatosha. Wakiipenda, dau unalo.

Nilifanikiwa kuongea na wajisiriamali wachache wa kitanzania ambao wamepokea hizo pesa tangu 2018 (sijapata wa 2017 kwenda nyuma), na wana shuhuda nzuri.

Kwa ufupi, ni hivi:
  1. Wewe una idea yako, ambayo ikiwezeshwa itazalisha mali. Au una biashara ambayo haina zaidi ya miaka 3 tangu kusajiliwa.
  2. Wewe ni mtanzania (automatically mwafrika)
  3. Unaweza kujielezea vizuri, na kuwashawishi hawa wafadhili kwamba ukipewa pesa, utafanyia kitu
  4. Idea au biashara yako iwe na uwezo wa kuscale (yaani kukua kwa mapana na marefu, ikipewa muda na "mbolea"). Kumbuka kuwa milioni 10 sio hela ndogo. Kwa hiyo, lazima uwe na kitu ambacho kina uwezo wa kukua.
Kama hizo pointi hapo juu hazikusumbui, basi fursa hii ni kwa ajili yako...

Milango imefunguliwa kwa wajasiriamali wote ambao wanaamini wana idea itakayoifanya bara la Afrika kupiga hatua nyingine mbele. Tarehe ya mwisho ya kujiandikisha ni Jumapili, Januari 31, 2021.

Kwa habari zaidi, tembelea
 

Attachments

Naona ipo kama drama ya kikorea inayoitwa star up ndani kuna hawa watu wa the sand box kwa ajili ya kuinua vijana wajasiliamali
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Hii program yao nzuri sana, ndio ambayo hats yule jamaa wa zaidi enterprises alipata dola laki moja miaka michache iliyopita, hakika wana moyo wa kweli
 
Hii program yao nzuri sana, ndio ambayo hats yule jamaa wa zaidi enterprises alipata dola laki moja miaka michache iliyopita, hakika wana moyo wa kweli
Ni yakweli kwahiyo?
 
Back
Top Bottom