Top 10 ya michezo inayo lipa zaidi duniani

Top 10 ya michezo inayo lipa zaidi duniani

Papaa Gx

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2016
Posts
11,097
Reaction score
17,929
Nimekuwa nikipita katika jukwaa hili la michezo na mara nyingi nimekutana na habari za Simba na Yanga, ama mara nyingi limeegemea kwenye upande wa ligi ya nyumbani hasa mpira wa miguu. Nimeona leo niwape kitu tofauti kile ninacho kifahamu katika kufuatilia mambo. Binafsi napenda michezo, michezo ndio starehe yangu kubwa. Basketball na Tennis ndio michezo ninayo ipenda zaidi, ile kukaa na kuitizama naburudika sana.

Kama tujuavyo kipaji kinalipa na kukupa umaarufu sana. Basi kupitia kipaji watu wamevifanya kuwa professional na kuwalipa mamilioni ya hela. Huenda utakuwa unafahamu ama hufahamu basi hii ndio orodha ya michezo inayo lipa zaidi duniani.

1. Basketball

Mchezo wa Basketball ndio unaongoza kulipa zaidi katika nyanja ya michezo. Ligi Maarufu na inayo lipa zaidi duniani ni NBA ya Marekani. Asilimia kubwa ya mchezaji wa Basketball ndoto na malengo yake makubwa ni kucheza NBA. Basketball inakuwa ndio mchezo unaolipa zaidi kutoka na malipo ya $343 millioni sawa na Tsh 798,504,000,000 kwa mwaka. Hayo ndio malipo aliyo pokea mchezaji wa Basketball pamoja na endorsement. Na mchezaji tajiri zaidi katika mchezo huu ni Michael Jordan na pia ndio mwanamichezo tajiri kuliko wote, anamiliki zaidi ya Dolla Billion 2.

2. Combat Sports

Combat sports inajumuisha michezo kama vile boxing, wrestling, muay Thai n.k. Boxing ndio maarufu katika mjumuiko huu, pambano linaloshikilia rekodi ya kulipa zaidi ni lile la $333 millioni sawa na Tsh 775,224,000,000 kwa pambano moja tu. Mchezaji tajiri zaidi katika mchezo huu ni Floyd Mayweather. Pambano maarufu na lililo tazamwa zaidi duniani ni lile la Floyd Mayweather dhidi ya Manny Pacquiao.

3. American Football

Mchezo huu unalipa zaidi na ndio mchezo unao tizamwa zaidi nchini Marekani. Una mamilioni ya mashabiki nchini Marekani, NFL ndio ligi maarufu na inayo lipa zaidi duniani. Kutokana na kulipa na umaarufu wake kila mchezaji wa American Football anatamani kucheza katika ligi hiyo. American Football ni maarufu zaidi katika nchi ya Marekani na Canada. Makusanyo ya $253 millioni sawa na Tsh 588,984,000,000 pamoja na endorsement kwa mwaka mmoja ndio anayo pokea mchezaji anae lipwa zaidi katika mchezo huo. Mchezaji tajiri zaidi katika mchezo huu ni Roger Staubach.

4. Golf

Golf ikiwa inaonekana ndio mchezo rahisi kujifunza lakini ni moja ya mchezo mgumu kupata umahiri. Mchezo wa golf ni maarufu zaidi Ulaya na Marekani. Golf pia ni mchezo maarufu duniani, mcheza golf alielipwa hela nyingi katika mchezo huo ni zaidi $127 millioni sawa na Tsh 295,656,000,000 pamoja na endorsement kwa mwaka mmoja. Mchezaji tajiri zaidi katika mchezo huu ni Tiger Woods.

5. Soccer

Soccer ndio mchezo maarufu zaidi duniani ukiwa na zaidi ya bilioni 4 ya mashabiki katika kila pande ya dunia. Na pia ni moja mchezo unao chezwa zaidi duniani kwa angalau kila taifa. Malipo ya zaidi $126 millioni sawa na Tsh 293,328,000,000 pamoja na endorsement kwa mwaka mmoja yanafanya kuwa mchezo unaolipa zaidi katika nafasi ya 5. Mchezaji tajiri zaidi katika mchezo huu ni Mnyama Cristiano Ronaldo CR7. Na ndio mcheza soccer billionea wa kwanza duniani. Ligi Maarufu katika mchezo huu ni UEFA Champions League, FIFA World Cup na Euro Cup.

6. Tennis

Tennis ni moja mchezo maarufu duniani kwa sasa, ni mchezo wenye mamilioni ya mashabiki duniani. Kama serikali yetu ingekuwa na sera nzuri katika mchezo huu basi mimi hapa Papaa Gx ningekuwa mcheza tennis maarufu duniani. Huu mchezo ndio kipaji changu nilicho tunukiwa na ninaupenda sana. Mcheza tennis anaelipwa zaidi katika mchezo huo mpaka sasa anapokea zaidi ya $106 millioni sawa na Tsh 246,768,000,000 pamoja na endorsement kwa mwaka mmoja. Mchezaji tajiri zaidi katika mchezo huu ni Roger Federer, wacheza Tennis endorsement zao ndio huwa za gharama zaidi kuliko pesa wanazo pokea kwenye michuano. Michuano maarufu zaidi ni French Open (Roland Garros), Wimbledon, US Open na Australian Open.

7. Ice Hockey

Ice Hockey ni mchezo maarufu na unaotizamwa zaidi nchini Marekani. Ligi maarufu na inayo lipa zaidi duniani ni NHL ya Marekani, kutokana na malipo hayo imeufanya mchezo huu kushika nafasi ya 7. Mchezaji aliyelipwa zaidi alipokea zaidi ya $99 millioni sawa na Tsh 230,472,000,000 pamoja na endorsement kwa mwaka mmoja. Mchezaji tajiri zaidi katika mchezo huu ni Wayne Gretzky

8. Baseball

Mchezo wa baseball unashika nafasi ya 8 katika orodha ya michezo inayo lipa zaidi duniani. Baseball ni maarufu zaidi nchini Marekani na ligi maarufu duniani ni MLB ya Marekani. Kila mcheza baseball anatamani kufika katika ligi ya Marekani (MLB) maana ni ligi inayolipa zaidi. Mchezaji alielipwa zaidi katika historia ya mchezo huo alipokea malipo ya zaidi $38 milioni sawa na Tsh 88,464,000,000 pamoja na endorsement kwa mwaka mmoja. Mchezaji mwenye utajiri zaidi katika mchezo huu ni Alex Rodriguez.

9. Auto Racing

Auto racing imejumuisha kama mashindano ya Formula 1 ni mchezo wenye umaarufu zaidi Ulaya na Marekani. Mchezo huu wa ajabu ni moja ya mchezo wa hatari zaidi, ni mchezo wenye ustadi na kuvutia. Kiwango cha juu alicho lipwa dereva wa Formula 1 ni $18 millioni sawa na Tsh 41,904,000,000 kwa mmoja. Mchezaji tajiri zaidi katika mchezo huu ni Michael Schumacher.

10. Cycling

Kuendesha Baiskeli ni mchezo unaolipa zaidi katika nafasi ya 10. Miaka 123 iliyopita Charles Minthorn alikuwa muendesha baiskeli wa kwanza kuendesha umbali wa maili moja chini ya dakika 1 mwaka 1899. Lance Armstrong alishika nafasi ya 9 katika orodha ya wanamichezo tajiri zaidi mwaka 2010 katika jarida la Forbes akikusanya zaidi ya $28 millioni sawa na Tsh 65,184,000,000 kwa mwaka huo.

Hiyo ndio orodha ya michezo inayo lipa zaidi duniani, ningeshauri watu wawekeze kwa namna yoyote ile katika kipaji. Kipaji kinalipa sana tena sana.

Mkono wa Papaa Gx.
 
Ule mchezo wa utamu utamu upo nafasi ya ngapi katika top HANDRED. [emoji23]

Ule ndio mchezo pendwa ambao soote tunashiriki, sisi wa kimoja chali, wale wasimamia ukucha n.k woote tumo[emoji23]
Dah aisee tunawaza ngono masaa 24
 
Papaa me naanza kubet basketball naachana na soccer wamenichania Sana mikeka..ngoja nijaribu mchezo wa kitajiri huenda ndo ukawa na pesa nyingi.
 
Kwanini CR7 na si Messi? Messi pamoja na mshahara wa €1,200,000 kwa wiki bado amezidiwa na huyo jamaa?
 
IMG-20220702-WA0016.jpg
 
Football is the richest sport in the world with a Net Worth of around $600 Billion. Football is played by around 250 million people, often known as soccer, throughout 200 nations around the world. It is one of the most well-known sports, with a $600 billion global market value.6 Jun 2022
 
The NBA leads in average player salaries by a wide margin, as evidenced by Statista's list that also includes average 2019-2020 player salaries for the MLB, NFL, NHL and the MLS: Average NBA salary: $8.32 million. Average MLB salary: $4.03 million. Average NFL salary: $3.26 million.
 
Ni sahihi ila ndugu ndege John, Basketball ndio mchezo unaolipa zaidi katika mchezo yoyote duniani. Yaani wachezaji wa Basketball wanalipwa pesa nyingi kuliko wa Football. Na NBA ndio ligi inayolipa zaidi wachezaji wake.

Stephen Curry ndio analipwa zaidi NBA analipwa zaidi ya $48 sawa na Tsh 111,744,000,000 kwa mwaka hiyo ni bado hujaweka malipo ya endorsement.

Nikola Jokic wa Denver Nuggets amesaini mkataba mpya wa miaka 5 utakao mfanya apokee $270 millioni sawa na Tsh 628,560,000,000. Mkataba huu utamfanya awe mchezaji anae lipwa zaidi katika NBA.
Football is the richest sport in the world with a Net Worth of around $600 Billion. Football is played by around 250 million people, often known as soccer, throughout 200 nations around the world. It is one of the most well-known sports, with a $600 billion global market value.6 Jun 2022
 
Hahaaaa, mkuu siungi mkono masuala ya kubashiri alimaarufu kubet. Ila kama utaka kuanza kubet kwenye Basketball unaweza anza ana michuano ya NBA Summer League inayotarajia kuanza usiku wa leo. Michuano ya Summer League ipo kwa lengo la kuwapa vijana ama wale walikosa muda wa kushiriki katika msimu husika wa NBA.

Pia mkuu kuna michuano ya Wimbledon katika Tennis inaendelea
Papaa me naanza kubet basketball naachana na soccer wamenichania Sana mikeka..ngoja nijaribu mchezo wa kitajiri huenda ndo ukawa na pesa nyingi.
 
Swali zuri sana, mkuu endorsement ndio zinafanya awe juu yake zaidi. CR7 ana mikakati minono ya endorsement kuliko Messi. Na kitu kingine hawa wanamichezo wanalipwa zaidi na endorsement zao tofauti na mishahara wanayo pokea.

Mtu kama Roger Federer analipwa zaidi na endorsement kuliko gawio analo pata kwenye Tennis. Kwa mwaka huu amepata gawio la $0.7 millioni sawa na Tsh 1,629,600,000 wakati kwenye endorsement ana mkataba wa $90 millioni sawa na Tsh 209,520,000,000. Federer ndio mcheza tennis anaelipwa zaidi katika mchezo huo wakati huo huo ni anashika nafasi ya 7 kwa ujumla wa wanamichezo wote kwa wanao lipwa zaidi.

Hawa jamaa wanatengeneza pesa zaidi kwenye matangazo ya bidhaa mbalimbali, huku kwenye vipaji wanasaka umaarufu tu kisha wakusanye mamilioni ya hela kwenye matangazo.
Kwanini CR7 na si Messi? Messi pamoja na mshahara wa €1,200,000 kwa wiki bado amezidiwa na huyo jamaa?
 
Swali zuri sana, mkuu endorsement ndio zinafanya awe juu yake zaidi. CR7 ana mikakati minono ya endorsement kuliko Messi. Na kitu kingine hawa wanamichezo wanalipwa zaidi na endorsement zao tofauti na mishahara wanayo pokea.

Mtu kama Roger Federer analipwa zaidi na endorsement kuliko gawio analo pata kwenye Tennis. Kwa mwaka huu amepata gawio la $0.7 millioni sawa na Tsh 1,629,600,000 wakati kwenye endorsement ana mkataba wa $90 millioni sawa na Tsh 209,520,000,000. Federer ndio mcheza tennis anaelipwa zaidi katika mchezo huo wakati huo huo ni anashika nafasi ya 7 kwa ujumla wa wanamichezo wote kwa wanao lipwa zaidi.

Hawa jamaa wanatengeneza pesa zaidi kwenye matangazo ya bidhaa mbalimbali, huku kwenye vipaji wanasaka umaarufu tu kisha wakusanye mamilioni ya hela kwenye matangazo.
Uko nondo mzee
 
Ni kweli basket inalipa sana kuliko footbal lakini footbal ndo mchezo unaongoza kwa kupendwa hapa duniani. Hii ni kutokana na maskini na matajiri kupenda mpira wa miguu
 
Sahihi kabisa, soccer unaopedwa na maarufu zaidi pia ndio wenye mashabiki wengi zaidi. Soccer una zaidi ya mashabiki billioni 4 duniani, Cricket unashika nafasi ya 2 kwa kuwa na mashabiki wengi ukiwa na zaidi ya mashabiki billioni 2.5 duniani na namba tatu ni Basketball ukiwa na mashabiki zaidi ya 2.4 bilioni duniani.
Ni kweli basket inalipa sana kuliko footbal lakini footbal ndo mchezo unaongoza kwa kupendwa hapa duniani. Hii ni kutokana na maskini na matajiri kupenda mpira wa miguu
 
5. Soccer

Soccer ndio mchezo maarufu zaidi duniani ukiwa na zaidi ya bilioni 4 ya mashabiki katika kila pande ya dunia. Na pia ni moja mchezo unao chezwa zaidi duniani kwa angalau kila taifa. Malipo ya zaidi $126 millioni sawa na Tsh 293,328,000,000 pamoja na endorsement kwa mwaka mmoja yanafanya kuwa mchezo unaolipa zaidi katika nafasi ya 5. Mchezaji tajiri zaidi katika mchezo huu ni Mnyama Cristiano Ronaldo CR7. Na ndio mcheza soccer billionea wa kwanza duniani. Ligi Maarufu katika mchezo huu ni UEFA Champions League, FIFA World Cup na Euro Cup.

Kumbe wewe ni Shabiki wa ronaldo 😁 eti mnyama
 
Back
Top Bottom