Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
TOP GUN GRUMMAN F-11 SUPERSONIC FIGHTER & STORY OF A TIGER WHO HAD BITTEN ITS OWN TAIL: Ndege vita iliyojipiga yenyewe kwa kukimbia speed kuzidi kombora lake.
UTANGULIZI: Jaribu kujenga picha ya kwamba Morani wa kimasai anarusha mkuki (mkuki wenye ncha kali mbele na nyuma) mita kadhaa mbele ili amchome simba.
Baada ya kuurusha mkuki ule anaanza tena kuukimbilia kabla haujatua mwilini mwa simba na kwa bahati mbaya anajichoma yeye mwenyewe katika mkuki aliourusha mwanzo.
Sasa jiulize huyu morani anauwezo wa kukimbia kwa speed ya ajabu kiasi gani? Hii ndio Supersonic Speed. Kukimbia kuzidi mwendo wa sauti.
BACK TO THE STORY: Mpaka kufikia miaka ya 1950s, vita baridi baina ya USSR (The eastern bloc) pamoja na USA (The western bloc) ilikuwa imepamba moto sana na Soviets walikuwa wanaonekana wapo vizuri sana katika suala zima la teknolojia ya utengenezaji wa ndege vita. USSR walikuja na toleo jipya kabisa la ndege aina ya MiG-15.
HII NDIO MiG-15 ya USSR
Hii ndege mpya ilikuwa ina muundo mpya ambao hakuna mtu yeyote aliwahi kuona ikiruka. Mabawa yake ya nyuma yaliyochongwa kwa ustadi wa hali ya juu sana yaliiwezesha ndege hii kuweka kukimbia kwa speed ya ajabu ambayo ingeweza kukaribia speed ya sauti (Supersonic Speed).
Ndege hii pia ilikuwa na ufanisi wa ajabu sana ukilinganisha na ndege zingine zooote za wakati huo. Jeshi la anga la Marekani lilipaswa kuumiza kichwa na kung'amua namna njema ya kupambana nayo ili kuweza kulinda heshima yao ya "air superiority" na kulinda ndege zao.
Katika kufanikisha hilo, wakaamua kuifuata kampuni ya kutengeneza silaha na vifaa vya kijeshi (Defence Contractor) ya Grumman ambayo punde tu ikafanya maunjanja ya kutaka kuizidi ndege mpya ya USSR aina ya MiG. Kilichofuata katika project ya Grumman ni F-11 Tiger, dege ambalo lilijumuisha technology za kisasa na za juu kabisa katika tasnia ya "naval aviation" na kutaka kufanana na dege lingine aina ya F9F Cougar.
HII NDIO F9F COUGAR
Hizi ndege aina ya Cougar zilikuwa na mabawa yaliyokuwa na uwezo wa kukata upepo kwa mtindo wa kipekee wa aina yake, lakini ndege aina ya Mig-15 zilikuwa zimezidi kwa mbali ndege ambazo mabawa yake yalikuwa yamenyooka (straight wing fighters) katika vita ya Korea. Jeshi la anga la Marekani lilihitaji aina fulani ya ndege ambazo zingeweza kulinda meli zake wakati zinapambana na ndege za adui huko angani.
Kampuni ya Grumman ilianza jitihada zake na ndege ya F9F Cougar, ila wakaamua kurudi katika ubao wao wa mchoro na kuamua kuja na hiyo F-11 Tiger, ndege iliyokuwa ikikimbia kwa speed ya sauti, ambayo ilikuwa na uwezo wa kuruka kutoka katika manowari na kuweza kupambana na MiG za wasoviet. Kwa bahati mbaya sana, kutokana na mwendo wake wa ajabu ndege hiyo ndio ikawa ndege vita ya kwanza kabisa kujilipua yenyewe.
Mnano tarehe 21 mwezi wa September mwaka 1956, rubani aliyekuwa akitumika kujaribu ndege (Test Pilot) bwana Tom Attridge alianza kuruka mdogo mdogo kimo cha chini akiwa katika dege lake hilo la Tiger. Akiwa katika mruko huo, alifyatua makombora mawili kutoka katika ubavu wa kulia na kushoto wa ndege na hakuweza kuhisi kitu chochote mpaka pale alipofika mwisho wa mruko wake na yake makombora kuanza kukwangua ndege yake.
Alianza akiwa katika umbali wa futi 20,000 na kisha kushuka mpaka futi 17,000 alipokuwa anafyatua makombora. Aliserereka chini, mpaka futi 13,000 akaangusha makombora yaliyobaki katika mabawa ili ndege iwe nyepesi.
Bado rubani aliendelea kuserereka chini, lakini alipofika umbali wa futi 7,000, alisikia kitu kimepiga kioo cha mlangoni pake ile puuuuuh pamoja na moja ya engines za ndege. Ndege ilianza kupoteza nguvu na rubani bwana Attridge akawa anaipeleka kambini ili aweze kutua salama.
Lakini ili aweze kuiweka sawa (kwa maana ilikuwa imegeuka upside-down) pasipo kuvunja kioo cha mlangoni, alilazimika kupunguza speed mpaka mwisho na engine kuweza kuzalisha 78% tu ya nguvu yake ya kawaida. Angeweza kutua salama katika uwanja wa kambi kwa nguvu hiyo.
Miles 2 kutoka katika njia ya kutua ndege, engine ikazima ile mazima kabisa. Rubani Attridge hakukata tamaa kabisa - hao test pilots wengi wao huwa ni vichaa - katika ndege yenye mwendo mdogo alifanikiwa kutua katika miti.
Licha ya kupata majeraha kadhaa katika mwili wake, alifanikiwa kutoka katika ndege na kisha kubebwa na helicopter ya uokoaji. Ndege, kama ilivyokuja kujulikana baadae, ilipigwa na kombora lake lenyewe kwenye kioo cha mbele, engine ya upande wa kulia pamoja na kwenye pua.
KILICHOTOKEA
The low pitch of the plane and its trajectory, combined with the trajectory of the bullets and the speed of the Tiger's descent at half the speed of sound right into the guns' target area, meant that the plane would easily catch up with its own burst of 20mm fire.
The pilot shot himself down in about 11 seconds.
OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.