Top Three yako ni Ipi ? Yangu ni hii


Hata hao kina Ronaldo wanatetea mishahara yao, ndiyo maana muda wote wanalilia nyongeza za mishahara.

Siku hizi mchezaji ana team kubwa nyuma yake, kuanzia personal trainers, chefs, financial analysts, psychologist, designers etc ambao wote wako kwenye payroll yake.

So mchezaji ni business tosha, miaka hiyo karibia wachezaji wote walikuwa wanategemea timu peke yake kuprovide services kama hizo.
 
safi sana mtoa hoja hii ila nami niongezee hapa ni vema mno tukatumia jukwaa hili kuijulisha hii new generation yetu kwamba ni safi sana kwa mtu kuijua kwanza nchi yako au yanayokuzunguka kabla hujayajua ya mbali;wengi wetu humu hutujui kuwa nchi hii imeshawahi kuwa na wachezaji wengi tu wa mpira wenye vipaji ambao wengi wao vipaji hivi havikuwasaidia kutokana na mfumo mbaya tuliokuwa nao,wachezaji kama;Sunday Manara,Kassim Manara(huyu alikuwa akiweka mpira kati ya miguu yake kuuchukua ule mpira ufanye kazi ya ziada),Gagarino,Jela Mtagwa(sijui kama alilipwa hati miliki ya kutokea kwenye stamps),Omari Hussein,Ngulungu,Peter Tino,Mohammed Richard,Lumelezi,G.Masatu,(almost team yote ile ya Pamba) etc etc ,ni vema tukaanzia huku ndio tuendelee kuwajua wa huko south America ,Europe etc etc,du nimekumbushwa kuhusu KING KIBADENI na OMARI MAHADHI BIN JABIR(mfupi kiumbo ila pale kati kati ya goli kumfunga ilikuwa shida)na inasikitisha mpaka leo mfumo ni ule ule wachezaji wetu hawasogei mbele na waziri wetu anakimbizana na magazeti uchwara yanayomchafua mfalme!!
 
Nimemwona sana tu. Labda kama angetaka top 5 nadhani angekuwepo yeye na Edward Chumila

Lunya bwana ile namba naikubali... nadhani hata Mogella anasubiri
 
Italy unathubutu kumuacha Roberto Baggio?
 

Mfumo wetu wa soka umekua mbaya sana. Sijui tunakosea wapi wabongo sisi. Yaani TFF sijawahi kuona la msingi wanalofanya kuipromote ligi yetu na vipaji vya wachezaji wetu.
Something has to be done hii CAF yenyewe tunaenda kusindikiza tu huko maana kupita ilikua bahati tu. 😭😭
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…