Topic 2: Tathmini ya mapato ya kilimo cha michungwa 1000 baada ya miaka 3

Kahtan Ahmed

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
765
Reaction score
490
Habari wana JF,

Imepita muda tangu nitangaze wazo la kilimo cha biashara cha michungwa na tathmini ya mapato pamoja na gharama zake ingawa nimepata changamoto za maswali mengi kutoka kwa wanachama wa jf na lengo na dhumuni la ujio huu wa pili niliouita topic 2 ni kutokana na changamoto hizo nilizozipata kwa wale wageni wa topic hii marejeo ya topic ya kwanza ni https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-cha-michungwa-1000-baada-ya-miaka-3-a-7.html

Kama nilivyoeleza kua ujio huu wa pili ni kutokana na changamoto zilizojitokeza kwa wana JF.

Kuna baadhi ya mlio wengi mmevutiwa na thread hii na pia mlitamani muifanyie kazi na kuna wengine mlinipigia simu na kuna wengine tulionana ana kwa ana miche ila kwa bahati mbaya mimi nilikua sijajikita katika uzalishaji wa miche hii ya michungwa hivyo basi nikaamua rasmi kuanzisha project ya kupandikiza miche hii ya michungwa(grafting) katika shamba langu na kuamua kuwatangazia kuanzia kipindi hiki kua miche hiyo ninaizalisha mimi mwenyewe katika shamba langu.

Sifa za miche hiyo ya michungwa ni kama ifuatavyo:-

1. AINA YA GALATIA
2. ASILI : ISRAEL
3. UNAZAA MAPEMA (MIAKA 2)
4. UNAZAA MACHUNGWA MPAKA 4000 KWA MCHUNGWA
5. UNATOA MACHUNGWA MAKUBWA
6. UNATOA MACHUNGWA MATAMU
7. MACHUNGWA YENYE MAJI MENGI
8. RANGI YA MACHUNGWA INAVUTIA
9. MACHUNGWA MAGUMU(YANASAFIRIKA)
HIZI NI BAADHI YA PICHA ZA MICHUNGWA YENYE UMRI WA MIAKA MIWILI KATIKA SHAMBA LANGU LA MICHUNGWA ILOKO TANGA.



 

Attachments

  • IMG-20140222-WA002.jpg
    132.4 KB · Views: 834
  • IMG-20140222-WA005.jpg
    143.3 KB · Views: 354
  • IMG-20140222-WA015.jpg
    155.9 KB · Views: 799
Ongera mkuu!ila mkuu kuna machungwa yalikua yanatoka muhoro,yalikua makubwa na matamu unayoyafahamu
 
Kahtaan umeendeleza makosa yaleyale ya kusema machungwa 4000 badala 400. Mchungwa mnoja unatoa machungwa kati ya 600 hadi 800. Kama una utafiti unaosema machungwa 4000 basi weka hapa au weka link
 
mkuu muhadharusi sikuwahi kuona machungwa hayo ila ningeyaona ningejua ni mbegu gani
 
hemu google uangalia machungwa aina ya galatia
 
Tayari nimeanza kutekeleza mradi huo, lakini nipanda michungwa 1000 kwenye ekari 10 aina ya valencia
 
valnceia ni mazuri na yana uzao tatizo ya valencia yanaozea mtini kabla hata ya kukomaa
 



Michungwa yako ni ya aina gani.??
Maana kwenye thread yako ya mwanzo ulitaja aina nyingine.
 
Hebu piga picha huo mti wenye machungwa elf nne kurahisisha kazi?

Maans hapo naona machungwa ya kawaida.
 
Tulivyokuwa chuoni Nyegezi miaka ile tulikuwa na michungwa aina ya Washington navel ilikuwa inatoa machungwa matamu sana yasiyokuwa name mbegu. pia yalikuwa na maji mengi sana.
 
ventore ni aina la jina ambalo si la kitaalam na jina la kitaalamu la michungwa hiini galatia
najua watu wengine mmekosa za kufanya mnatafuta thread za watu mukosoe jamani hapa si sehemu ya mabishano ni thread ya tangazo la michungwa aina ya galatia au kiuswahilini ventore
 
ok hamna tatizo nitakupigia huo mche ambao unazaa machungwa 4000 ila usubiri sanna mana miche hiyo hapo ndio inaelekea kua miaka 2 sasa uzao kamili inategemea na maeneo sasa ikifika idadi ntakutumia picha rabda baada ya miaka 3 kuanzia ilipofika
 
Mkuu, inachukua miaka mingapi mpaka mti uanze kubeba machungwa elf4?
 
mti ukikomaa mpaka miaka 4 mpaka 5 na inategemea na maeneo ndio inaweza kuana kutoa idadi hiyo
 
kaka me naic so kweli, wandugu nimetafuta wauzaji wakubwa wa machungwa wananiambia machungwa 4000, ni pickup moja iliyojaa vzuri, salsa jaman huo MRI wakubeba machungwa pickup nzima..... labda mvule
 
kaka me naic so kweli, wandugu nimetafuta wauzaji wakubwa wa machungwa wananiambia machungwa 4000, ni pickup moja iliyojaa vzuri, salsa jaman huo MRI wakubeba machungwa pickup nzima..... labda mvule
true say
 
kaka me naic so kweli, wandugu nimetafuta wauzaji wakubwa wa machungwa wananiambia machungwa 4000, ni pickup moja iliyojaa vzuri, salsa jaman huo MRI wakubeba machungwa pickup nzima..... labda mvule

Wakuu tunavunjana mbavu, mvule tena?!!
Mimi nimejaribu kufanya research ya hiyo galatia lakini naona hilo jina hata halipo kwenye michungwa, huenda kuna jina lingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…