Total Political Dominance: Je, ni rahisi kushindana na CCM?

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,530
Reaction score
3,422
Habari JF ,
Kwa kuangalia muundo wa Katiba ya sasa na mapungufu yake , Rais akiwa pia Mwenyekiti wa CCM ambayo ni chama tawala , akiwa na mamlaka mbalimbali ya kikatiba na kiutendaji, hoja inajitokeza: je, mfumo huu hauleti hali ya “Total Political Dominance”?

Unapounganisha mamlaka ya Rais ndani ya Serikali na ushawishi wa nafasi ya Mwenyekiti wa chama tawala, mshindani wa kisiasa anakutana na nguvu kubwa sana ya kisiasa na kiutawala.

Swali kuu: Katika mazingira kama haya, ni kwa kiasi gani vyama vya upinzani vina nafasi halisi ya kushindana kwa usawa na CCM?

Je kuna haja ya kuwa na mfumo wa vyama vingi kwa katiba tuliyonayo?
 
My friends, ladies and gentlemen,

politics is a game of perceptions, game of numbers and ofcourse a game of interests.

ni kujipanga tu mazee bila kujiandaa kushindwa saikolojikali 🐒
 
Katiba na ccm vilianzishwa kwa pamoja 1977. Huwezi kuvitenganisha hivi vitu viwili hadi pale kimoja kati yao (ccm au katiba/au vyote) kife/vife.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…