Total yabadili jina sasa kuitwa TotalEnergies

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Kampuni ya Total, ambayo ndio kampuni kubwa ya Mafuta kwa nchi za Afrika Mashariki na ya 5 duniani, imebadili jina kutoka Total, na kuwa TotalEnergies.

Wewe kama mwana JF, be the first to know!.

Paskali.

 

Attachments

Nilikuwa naiomba hii kampuni kipindi wanajiita total nilikuwa bado sijazaliwa hivyo nilikuwa naomba hilo jina lirudiwe! lirudiwe...
 
Je, kwa mabadiliko hayo kuna athari zozote kwenye mapato yetu ya kodi?

Je, kampuni ya zamani ilikuwa na madeni ya kodi za zamani iliyo kuwa inadaiwa?

Maana siku za nyuma tulizoea kusikia kuwa njia moja wapo ya kukwepa kodi inayo daiwa kampuni ni kubadili jina la kampuni, sina hakika kama mchezo huo bado unaendelea.
 
Umeniwahi boss,hapo nahisi kuna miaka 10 ya kujaribu biashara afu ndio wa kodi
 
Kwenye mabadiliko ya jina hakuna athari yoyote kiuchumi kwenye mapato na kodi, kila kitu ni kile kile na vile vile isipokukuwa jina tuu ndio linabadilika.

Kubadili jina sio kubadili umiliki, hivyo kila kitu kiko vile vile kama ni madeni yapo na yanaendelea.

Kampuni ikibadili umiliki ndipo kuna malipo ya capital gain tax kampuni iliyonunua inatulipa.

Kutakuwa na athari tuu za kiuchumi za ndani, kugharimia kubadili zile Logo za vituo zaidi ya 100 nchini!.

P.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…