Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi
Makala yangu kwenye Nipashe ya leo
Anachofanya Rais Samia na serikali yake, kutenga asilimia fulani ya fedha za kila halmashauri, na kuzitoa kama mkopo nafuu usio na riba kwa wikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu, kinapaswa kuungwa mkono na makampuni yote yanayofanya biashara Tanzania, kupitia sera zao za kurejesha kwa jamii, CSR, ifike wakati sasa CSR isiwe ni hisani, au huruma bali iwe ni wajibu.
Mikopo ya wanawake vijana na wenye ulemavu, imepachikwa jina la Mikopo ya Mama Samia, ina lengo la kuwajengea uwezo kwa kuwapatia mikopo ya mitaji. Sera za CSR za makampuni kurejesha kwa jamii ni hisani, inapaswa itungiwe muongozo ili isiendelee kuwa ni hisani, bali iwe ni wajibu.
Juzi kati, nilikuwa mjini Geita, kwenye maonyesho ya rasilimali za madini Geita, mgodi wa GGM, umechangia shilingi milioni 200, kufanikisha maonyesho hayo, ukiangalia hizi milioni 200, zimefanyia nini, unaweza usiamini, sehemu kubwa zimetumika kwa posho, na kugharimia vyakula, vinywaji na vitafunwa, kwa jina jingine ni zimeishia tumboni street!
Serikali yetu ifike hatua hizi CSR, zisiwe ni hisani, na kufanyia chochote tuu hata kama fedha zote zitaishia tumboni street. Hebu fikiria hiyo milioni 200 ya GGM kama ingenunua madawati au vitanda mahospitalini, wapi ingekuwa na faida zaidi?.
Juzi Ijumaa nimehudhuria tukio la utoaji tunzo kwa washindi wa shindano la VIA Creative International nchini Tanzania, ambapo, sio tuu nimeguswa na kilichofanyika, bali ningetamani kama makampuni yote yanayofanya biashara Tanzania, yatarudisha kwa jamii kitu cha kuoekanika na cha kudumu ambacho kitaacha alama. Kama makampuni yote yangefanya kama TotalEnergy, tungekuwa mbali!
Hawa TotalEnergies, CSR yao, wanatoa fursa kwa jamii husika kujitathmini changamoto zao, kisha ndipo inajibu kwa kuzitekeleza hizo changamoto.
Nikatamani kama makampuni yote nchini yanayofanya biashara, yangefanya kama kinachofanywa na TotalEnergies Marketing Tanzania, kwenye CSR yake. Unakwenda kwa jamii na kuuliza changamoto zao, na kuzipatia ufumbuzi. Enzi za JPM, aliwahi kufuta hafla ya Mchapalo wa Bunge jipya na kuelekeza fedha zinunue vitanda hospitalini. Akafuta paredi ya uhuru, fedha zikakarabati barabara ya Moroco –Mwenge.
TotalEnergy Tanzania imeandaa shindano na shule iliyoshinda, Ubungo Makuburi, itapatiwa sio tuu zawadi, bali changamoto kuu ya shule yao, itajibiwa kwa kujengewa ukuta kuizunguka shule hiyo.
Shindano hilo la kimataifa la "VIA CREATIVE" ni shindano linalolenga wanafunzi wa shule za msingi wa miaka 4 -19 kwa lengo la kuwapatia elimu ya usalama barabarani kwa njia ya sanaa ya michoro, muziki, maigizo na mashairi na kisha kuwapa fursa wanafunzi hao kuelezea uleewa wao na mapendekezo yao ya usalama barabarani kwa njia ya michoro na maigizo.
VIA Creative ni mradi ulioanza mwaka 2022 ambao tangu mwaka huo zaidi ya wanafunzi 22,000 wamefikiwa na mradi huu na kuweza kujenga klabu za mabolozi wa usalama barabarani kwenye shule 100 jijini Dar es Salaam na Bagamoyo. Mwaka huu mradi huu wa VIA Creative umewafikia wanafunzi 6000 kutoka shule za msingi Makuburi, Ubungo NHC, Buza, Jangwani, Ugindoni na Uzuri zilizopo jijini Dar es salaam na kuendeleza uundaji wa klabu za mabalozi wa usalama barabarani.
Hafla ya kukabidhi tunzo kwa wanafunzi walioshinda kwenye msimu huu wa tatu wa VIA Creative ilifanyika kwenye ofisi za TotalEnegies Marketing Tanzania Limited jijini Dar es Salaam ambapo shule ya msingi ya Makuburi Primary school iliibuka mshindi wa kitaifa wa shindano lwa shindano hili na muwakilishi wa Tanzania kwenye ngazi ya kimataifa munamo mwezi Novemba 2024. Aidha shule hiyo pia itazawadiwa kwa kutimiziwa mapendekezo ambayo wanafunzi waliyaomba kwaajili ya kuboresha usalama wao barabarani kwa kupitia programu hii ya VIA Creative.
Akiongea kwenye ghafla hiyo, mkurugenzi mkuu wa TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, Mamadou Ngom alisema, “Tunayo furaha kubwa kuwa hapa leo tukusherehekea mafanikio ya mabalozi wetu wa usalama barabarani kupitia mradi wa VIA Creative amabo tumeshirikiana na Nafasi Art Space ambao wamekuwa wakiwapatia wanafunzi hawa elimu ya usalama barabarani kwa kupitia sanaa. Kupitia mradi huu tumeweza kuunda klabu za mabalozi barabarani 120, 20 kutoka kwenye kila shula. Pia wanafunzi hawa wameweza kutoa mapendekezo yao ya jinsi ambavyo usalama wao wa barabara unaweza kuboreshwa nasi tutatekeleza mapendekezo hayo kwa shule ya msingi ya Makuburi ambao ndio washindi wa kitaifa wa shindano hili kwa mwaka 2024.”
Mgeni rasmi, mkuu wa Idara ya Mafunzo ya Trafiki Kinondoni, A.S.P Rose Bernard Maira aliwapongeza TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, TotalEnergies Foundation Pamoja na Nafasi Art Space akisema, “Nawapongeze washika dau waliowezesha mradi huu wa VIA Creative, yani TotalEnergies Foundation, TotalEnergies Marketing Tanzania Limited Pamoja na Nafasi Art Space, juhudi zenu na mafanikio yenu katika kutoa elimu ya usalama barabarani zinastahili kupongezwa na kuigwa na makumpuni mengine ili kuchochea usalama wa Watoto wetu waendapo na watokapo mashuleni.
Aidha aliongeza kuwa “Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani tupo Pamoja nanyi kwenye jambo hili na katika kutoa elimu ya usalama barabarani pamoja na kuzijua sheria, kanuni na taratibu za barabarani kwa wanafunzi na watumia Barabara wote. Aidha, tumefurahia kujua kwamba mradi huu pia unalengo la kutimiza mapendekezo ya kuboresha hali ya usalama kwa wanafunzi wa shule iliyoshinda kama trulivyopata kuona kwenye filamu ya wanafunzi hao. Pia niwatakie kila la heri washindi hawa kwenye hatua nyingine ya shindano ambalo wanatarajia kuingia, nawasihi muiwakilishe Tanzania vizuri na mungae Pamoja na kushinda ngazi za shindano la VIA Creative zijazo.”
TotalEnergies ameonyesha njia, wengine wafuate, CSR isiwe ni hiyari, huruma au hisani, iwe ni wajibu!.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali