TotalEnergies U-20 Africa Cup of Nations (AFCON) CECAFA Qualifiers 2024

TotalEnergies U-20 Africa Cup of Nations (AFCON) CECAFA Qualifiers 2024

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
07 October 2024

MICHUANO YA KANDA YA CECAFA U-20 KUELEKEA FAINALI ZA AFCON YA U-20 INAENDELEA DAR ES SALAAM


View: https://m.youtube.com/watch?v=4u3RG9q7e7w Benchi la ufundi la Tanzania chini ya kocha mkuu Charles Boniface Mkwasa akisaidiwa na Kalimangonga Ongala, Juma Kaseja..


RISING Stars Jumapili walianza kampeni zao za kuwania ubingwa wa mashindano ya Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kwa kuinyoa wenyeji (Ngorongoro Heroes) Tanzania 2-1 katika uwanja wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Timu ya Tanzania U20 imepangwa katika Kundi A pamoja na Rwanda, Sudan, Kenya, na Djibouti.

1728346873221.png

Katika Kundi B, mabingwa watetezi wa CECAFA U20 Uganda wamepangwa pamoja na Sudan Kusini, Ethiopia, na Burundi. Uganda.

Matokeo :
Tanzania 1 - Kenya 2
Sudan 3 - Djibouti 1
South Sudan 0 - Burundi 1
Uganda 3 - Ethiopia 0


Mechi zifuatazo zitapigwa siku ya jumanne tarehe 8 October 2024 katika vijana vya KMCC, AZAM COMPLEX na ule wa JKT vyote jijini Dar es Salaam.

Ukanda wa Cecafa unatarajiwa kutoa timu mbili ambazo zitashiriki Kombe la Afrika (Afcon Under 20) na Kenya inapigania kuwa kati ya mataifa hayo.

Nchi ambayo itakuwa mwenyeji wa Kombe la Afrika Under 20 itafahamika mnamo Oktoba 22 wakati ambapo kutakuwa mkutano wa CAF, Addis Ababa Ethiopia.

Senegal ndio mabingwa watetezi wa kipute hicho ambacho kitashirikisha timu za ukanda wa Zoni ya Kati, Zoni ya Mashariki ya Kati, Kusini, Zoni ya Magharibi A na B, Kaskazini na Magharibi ya Kati.
 
Makocha wa timu ya taifa sijui wanateuliwa kwa vigezo gani, ili Uganda Wana mpira mkubwa.
 
Tanzania nikiangalia hawa U-20 sioni kama siku za mbele, timu kubwa za ligi ya Tanzania zinaweza kuwasajili, timu kubwa zitaendelea kusaka vipaji nje.

Siyo kwamba vipaji havipo vya ndani bali scouting kuwatambua waliopo hakuna. Vipaji vipo lakini hawafanyi jitihada kuwaibua wacheze timu za vijana za Tanzania.

Michezo hii kama wangeleta vipaji vilivyopo tunaona wanaonekana ulimwengu wakiwa wachanga kabisa wakachukuliwa na timu kubwa tajwa za ndani na za nje .
 
Back
Top Bottom