TotalEnergies watoa ufafanuzi video inaonyesha watu wakitengeneza 'Oil fake' ya kampuni yao

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Ufafanuzi Kuhusu Video Inayosambaa: Operesheni ya FCC Dhidi ya Bidhaa Bandia

Dar es Salaam, Februari 13, 2026 Total Energies Marketing Tanzania Limited inatoa ufafanuzi kuhusu muktadha wa video iliyosambaa mtandaoni ambayo inaonekana kuonyesha bidhaa bandia za vilainishi vya Total Energies zikitengenezwa.

Video hiyo imetokana na operesheni rasmi ya kusaka bidhaa bandia iliyoongozwa na Tume ya Ushindani (FCC), inayotekeleza maagizo ya Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na bidhaa zote bandia, ikiwemo vilainishi

Total Energies haikuhusika moja kwa moja katika operesheni hii maalum. Hata hivyo, tangu mwaka 2024, tumekuwa tukishirikiana kikamilifu na mamlaka za serikali, ikiwemo FCC, kusaidia kubaini na kuondoa bidhaa bandia za vilainishi vya Total Energies kutoka katika soko la Tanzania. Juhudi hizi zinazoendelea zinalenga kulinda wateja wetu na kuendeleza hadhi ya chapa yetu.

Soma Pia: Video: Wakamatwa wakitengeneza 'Oil fake' za TotalEnergies

Aidha, tunapenda kuwahakikishia wateja wetu wote kwamba bidhaa halisi za Total Energies zinapatikana katika vituo vyetu vya mafuta na kwa mawakala walioidhinishwa nchini kote. Hatua kama zile zinazochukuliwa na FCC ni muhimu katika kuhakikisha kuwa wateja wanapata bidhaa salama, zenye ubora wa hali ya juu, na wanalindwa dhidi ya bidhaa bandia.

Total Energies itaendelea kushirikiana kwa karibu na mamlaka husika na washirika wengine katika kupambana na bidhaa bandia. Kipaumbele chetu ni kuwalinda wateja wetu na kuwezesha upatikanaji wa vilainishi halisi vya Total Energies.

Programu ya "kuskanisha" QR Code ili kutambua uhalisia wa bidhaa zetu:

Kwaajili ya kuwalinda wateja wetu, Total Energies ilizindua kampeni ya "kuskanisha" QR Code ili kutambua uhalisia wa bidhaa zetu. Hii ni njia rahisi, salama, na ya haraka ya kuthibitisha uhalisia wa vilainishi vyote vya Total Energies kabla ya kununua.
Jinsi ya Kutumia QR Code ili kutambua uhalisia wa bidhaa zetu:
1. Tafuta QR Code kwenye lebo ya mbele ya bidhaa ya vilainishi vya Total Energies.
2. Skanisha QR Code hiyo kwa kutumia kamera ya simu yako.
3. Subiri sekunde chache wakati mfumo unafanya uthibitisho.
4. Pokea Ujumbe wa Uthibitisho wa uhalisia wa bidhaa utakaojitokeza kwenye simu yako.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia 0800750242.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…