Chibule
Senior Member
- Sep 25, 2024
- 171
- 230
Napata wakati mgumu kuelewa kwa nini baadhi ya watu na vyombo vya habari vinasema TOTO AFYA KADI imeboreshwa au kurudishwa.
Inaonekana wengi hawajui nini kimetokea, labda acha niwakumbushe kidogo nini kimetokea.
Tanzania kupitia sera ya bima ya afya, NHIF kama zilivyo bima nyingine wakaboresha huduma zao na kuanzisha TOTO afya kadi tarehe 31 Julai 2017 siku ya jumatatu walizindua hii bima ya afya kwa watoto wote walio chini ya miaka 18, nakumbuka ilikua viwanja wa Mnazi mmoja na mgeni rasmi alikua waziri wa afya wa wakati huo, Mhe. Ummy Mwalimu na gharama ya kujiandikisha ilikua Tzs 50,400/= tu kwa mtoto mmoja kwa mwaka.
Mwaka jana (2023) NHIF kwa sababu walizosema kuwa mfuko umeelemewa na madeni kwa sababu watoto wanaotibiwa ni wengi wakati wanaochangia ni wachache, wakabadilisha utaratibu wa TOTO afya kadi, wakasema kuanzia tarehe 13 March, 2023 watoto wote wataanza kusajiliwa kupitia shule zao wanazosoma na sio mzazi kulipia bima moja kwa moja na wakaweka sharti kuwa, pale shuleni, mwalimu mkuu ataruhusiwa kusajili bima hii ya toto afya kadi kama akiweza kukusanya watoto 100 na sio chini ya hapo, kwaiyo, mzazi hawezi kusajili bima ya mtoto wake moja kwa moja, inatakiwa atoe taarifa aandikishwe, wakifika 100 basi NHIF wanakuja kusajili watoto hao pale shuleni.
Shida ikaja, watoto wanaoanza shule ni lazima wawe na miaka 7, hawa walio chini ya umri huu itakuaje? NHIF wakasema, watoto wote chini ya umri wa kusoma wakatiwe bima za afya kupitia wazazi wao, kumbuka mzazi mmoja kukata bima yake kwa kifurushi cha chini ilikua 192,000, akitaka amuweke na mke wake/mpenzi anaongeza pesa inakua 384,000 kwa hiki kifurushi cha chini, kwaiyo mzazi aliyekua na mtoto mmoja mwenye umri 0 mpaka miaka 6 alikua anajikatia yeye bima ya 192,000 kisha anamkatia mtoto 50,400 jumla inakua 242,400 kwa mwaka, na kwa mtoto alikua anamkatia moja kwa moja ofisi za NHIF.
Sasa huu utaratibu mpya walioweka NHIF ilitakiwa mzazi mmoja na mtoto mmoja aliye chini ya umri wa shule ambao kwa mwaka walitakiwa kulipa 242,400 inabidi sasa walipe 312,000 kwa mwaka, na zaidi kama mtoto yupo shule, huwezi tu kuamua kumkatia bima, inabidi mzazi ujisajili shule, kisha usubiri watoto 100 ndio msajiliwe.
Hapa watu wakaanza kupiga kelele. Sasa NHIF baada ya muda, wameamua kuondoa hiki kipengele kuwa shule lazima wafike watoto 100 ndio wasajiliwe, sasa hizi wazazi hata mkifika 10 basi mnasajiliwa, LAKINI BADO HAWAJASEMA KAMA MZAZI MMOJA UNAWEZA KUSAJILI MTOTO WAKO MMOJA.
Japo wamelegeza sharti hili, maana hawajaliondoa, bado watoto wasio na umri wa shule hawapati huduma kupitia TOTO AFYA KADI, mtoto aliye chini ya umri wa kusoma huwezi kumkatia TOTO AFYA KADI japo ni mtoto, inabidi ulazimike kukata bima ambayo na wewe mzazi upo kwenye kifurushi hicho, mfano kwa kifurushi cha chini kabisa, ukiwa mzazi mmoja na mtoto mmoja inakua 312,000 na mkiwa wazazi wawili na mtoto mmoja inakua 504,000, yani lazima na mzazi ukate bima hata kama hutaki.
Shida nyingine, toto afya kadi ilimpa mtoto uwanja mpana wa matibabu tofauti na huu utaratibu wa kupitia mzazi kwa maana mzazi ana madaraja ya bima na hata huduma zinatofautiana kwa kila daraja au aina ya bima anayokata.
Mfano, mzazi mmoja na mtoto mmoja anayelipia NAJALI AFYA ya 312,000 hawezi kufanana na mzazi mmoja mwenye mtoto mmoja anayelipia WEKEZA AFYA 576,000 na hata huyu hawezi kulingana huduma na mzazi mwenye mtoto mmoja anayelipia TIMIZA AFYA kwa 792,000.
Na hapo bado vifurushi vinapanda kulingana na umri, mzazi akivuka miaka 35 bei inapanda kutoka 312,000 kwenda 360,000 kwa NAJALI, 648,000 kwa WEKEZA na 888,000 kwa TIMIZA.
Ingawa NHIF imelegeza baadhi ya masharti, changamoto za msingi bado zipo.