Bishop Hiluka
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 7,147
- 14,699
Jana Ijumaa Novemba 17, 2017 Salvatore (Totò) Riina, bosi wa kikwelikweli aliyebatizwa jina la utani la Belva au Beast (Mnyama) alifariki dunia akiwa gerezani.
Totò Riina alizaliwa Jumapili ya Novemba 16, 1930, alikuwa mafia wa Kiitaliano na mkuu wa kundi la Mafia katika kisiwa cha Sisilia, lililojulikana kwa kampeni ya mauaji ya ukatili ambayo yalifikia kilele katika miaka ya 90, wakati vifo vya waendesha mashitaka wa Tume ya Kupinga Mafia, Giovanni Falcone na Paolo Borsellino vilisababisha chuki ya umma na msako mkali.
Mbali ya jina utani la Belva pia alijulikana kwa jina la Il Capo Dei Capi (Bosi wa mabosi). Bosi huyu ambaye alikuwa anajulikana kwa balaa zake kiasi cha kuitwa Mnyama.
Riina amekufa jana Novemba 17, 2017 kwa ugonjwa wa kansa akiwa na umri wa miaka 87 akiwa gerezani huko Parma.
Riina alikuwa anatumikia miaka 26 baada ya kupatikana na hatia katika tuhuma mbalimbali lakini ikiaminika kuwa alikuwa ameagiza vifo vya watu 150 wanaokwamisha mambo ya familia hiyo ya kimafia.
Akiwa mkuu wa koo inayoogopwa sana ya Mafia ya Cosa Nostra, na alisakwa kwa udi na uvumba kabla ya kutiwa mbaroni mwaka 1993 na kufungwa. Pamoja na kufungwa kwake alikuwa bado ana power na alitoa maagizo ya kuua akiwa jela...
=========================================
UPDATES:
Totò Riina aliua wapinzani wake wote.
Mtoto wa kiume wa Totò Riina alikuwa na umri wa miaka 17 wakati baba yake alipomuamuru kumteka na kumnyonga mfanyabiashara mmoja - mauaji ambayo yangeonyesha kuingia rasmi kwa kijana huyo ndani ya Cosa Nostra.
Ulikuwa mfano mmoja tu wa utawala wa mkono wa chuma/ kiuaji wa Riina ndani ya Cosa Nostra (kundi hatari la mafia), Riina aliyefia katika kitanda cha hospitali ya gereza asubuhi ya Ijumaa (jana), alifanya unyama nchini Italia kwa karibu miongo minne akiwa "bosi wa mabosi" wa kundi la mafia wa Sisilian.
Alipachikwa jina la "Mnyama" kwa sababu ya ukatili wake, alikuwa mhalifu asiyeogopa wala kujutia uhalifu wake, ambaye siyo tu aliwaua wapinzani wake kwa kiwango cha kipekee katika miaka ya 1980 na 90, lakini pia waendesha mashitaka, waandishi wa habari, na majaji ambao walitaka kuingilia nyendo zake.
Kundi la Mafia wa Sisilian kwa sasa limeachwa dhaifu baada ya kifo chake, wamechanganyikiwa, Riina alikuwa akiliongoza na akitafuta kushinda kutokea gerezani huko Parma alikokuwa amefungwa.
Lakini Umoja wa wahalifu hao bado upo, na bado wanajaribu kuyashepu maisha ya watu wao kijamii na kiuchumi katika sehemu za Sicily, lakini ni kama kimebaki kivuli tu cha kile kilichokuwa hapo awali, wakiwa wamedhoofishwa na polisi wa Italia na waendesha mashitaka na sidhani kama wataweza kurejesha tena power waliyokuwa nayo katika biashara haramu ya dawa za kulevya.
Kwa kifupi yeyote aliyethubutu kutaka kumshinda Riina, alifanywa kuwa victim wake mpya, kama ilivyokuwa kwa Giovanni Falcone, jaji aliyepambana na mafia aliyeuawa kwa bomu lililotegwa ndani ya gari kwa amri ya Riina mwaka 1992.
“Kifo cha Riina kinaonesha mwisho wa zama,” anasema Federico Varese, mtaalamu wa masuala ya mafia katika Chuo Kikuu cha Oxford.
"Unaweza kumlinganisha na [bosi wa dawa za kulevya wa Colombia] Pablo Escobar. Wote wawili walizindua mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya serikali na ambayo yalianzisha mshikemshike usiosahaulika."
Riina alikuwa akitumikia hukumu tofauti za maisha baada ya kuhukumiwa kwa kuamuru mauaji ya watu 150, ingawa wataalamu wanaamini kuwa idadi halisi ilikuwa kubwa zaidi ya hiyo.
Katika jiji lake la kuzaliwa la Corleone, palifanywa kama ngome ya mafia na kifo cha Riina kimewachanganya. Kuna pande mbili, vijana wanakiona kifo hicho kama nafasi nzuri ya mji huo kuachana na sifa yake mbaya, wazee wanamuenzi na kumkumbuka Riina wakimwelezea bosi huyo wa mafia kama mtu muungwana.
"Wakati Riina alipokuwa hapa, kila mtu alikuwa na kazi hapa Corleone," anasema Paolo, 77. "Watu hawa walitupatia kazi. Nilimjua. Nilimjua vizuri sana. Leo ni siku kama siku nyingine kama unavyoweza kuona. Lakini si siku ya kusherehekea."
Riina aliibuka katikati ya miaka ya 1970, alipokuwa kiongozi wa de facto wa familia ya uhalifu wa Corleone. Sicily ilikuwa ni kitovu cha biashara ya heroin ndani ya Marekani kufuatia vita vya Vietnam, na Riina akaanza kuogelea kwenye maisha ya kifahari kutokana na biashara haramu huku akitafuta namna ya kuwashinda wapinzani wake huko Palermo.
“Aliunda ushirikiano mpya na akaanzisha mapigano yaliyomwaga damu kwa kutumia vikosi vyake alivyoiita vya kifo,” anasema John Dickie, mtaalamu wa masuala ya mafia na mwandishi wa Mafia Republic. "Aliua wapinzani wake. Aliwaua wote, kwa mamia, aliamua kujisafishia njia ndani ya Palermo," alisema Dickie.
Mario Frances alikuwa mwandishi wa habari wa kwanza kufichua mambo ya Riina na Corleonesi ndani ya mafia wa Sicilian na aliuawa mwaka 1979. "Sikuwahi kujilipizia kisasi kwa kifo cha baba yangu, bali haki tu ndiyo itachukua mkondo wake," mwanawe, Giulio, alisema jana Ijumaa baada ya kupata taarifa za kifo cha Riina.
Wakati mabosi wengine wa mafia walikuwa pia wakatili lakini muda fulani walijichanganya na watu, Riina hakuwa na mpango wa kutaka kudumisha amani, na hakutaka kuwa na ukaribu wala uhusiano wa karibu na wanasiasa.
Mmoja wa victims wake alikuwa Piersanti Mattarella, rais wa Sicily, ambaye alipigwa risasi na kufa ndani ya gari lake mwaka 1980. Ndugu yake, Sergio, kwa sasa ndiye mkuu wa nchi ya Italia.
Kuongezeka kwa kiwango cha vurugu na unyanyasaji kulisababishwa na Riina kuamuru mauaji ya kikatili ya mvulana mwenye umri wa miaka 13 aliyekuwa ametekwa nyara, kunyongwa, na kutupwa ndani ya asidi, ikiwa ni ujumbe maalumu kwa wale wote ambao wangeweza kwenda kinyume dhidi yake - na nchi ya Italia ililazimika kujibu mapigo kwa kile kilichojulikana kama Maxi trial (mfululizo wa kesi zilizoanzia mwaka 1986 zikiwalenga mafia), zilisababisha mashtaka ya karibu mafioso 500, wengi wao walihukumiwa vifungo vya maisha ya gerezani. Kesi ziliwakilisha uthibitisho rasmi wa jinsi mafia walivyoenea sana huko Sicily.
Riina alijibu mapigo kwa nguvu kali: akiagiza mauaji ya Falcone na, miezi miwili baadaye, jaji mwingine, Paolo Borsellino, akauawa. Pia Riina alivamia Italia kama jitihada za kuidhibiti serikali. Lakini haikuwa.
Riina alikamatwa huko Palermo mwaka 1993. Ijapokuwa Riina alikuwa chini ya ulinzi maalumu wakipanga kudhoofisha nguvu zake za kuwasiliana na wenzake kutokea gerezani, lakini bado alifanya jitihada, na kamwe hakuachia uongozi wake kama ‘bosi wa mabosi’.
Mnamo Julai, ugonjwa wa saratani ulipomdhoofisha sana na hali kuwa mbaya zaidi, mahakama ilikataa ombi la familia yake kumhamishia nyumbani Sicily. Madaktari walisema kuwa alikuwa bado ana influence.
"Hawatanifanya nishindwe kusonga mbele, hata kama wanifunga miaka 3,000," alisema Riina.
Wapinzani wengi wa Riina walikimbilia Marekani kipindi Riina anafanya uhalifu na kuagiza mauaji, baadhi yao wamerudi ili kujaribu kuanzisha tena utawala wa Cosa Nostra.
Mara ya mwisho kamati ya uongozi wa mtandao wa uhalifu kukutana ilikuwa mwaka 1993.