Tottenham Hotspur wanaweza amua hatima ya Mourinho, lakini United wanachekelea rekodi hizi

marcoveratti

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
1,019
Reaction score
1,824
Ni hivi! Wakati Pep Gurdiola anajiunga na Manchester City watu waliamini mtu pekee ambaye anaweza kuwa mshindani wake ni Jose Mourinho kutokana na historia baina ya watu hao wawili.

Lakini baadae ikaanza kuonekana kama Mourinho na Pep ni watu wawili ambao wako dunia tofauti, huku Pep akiendelea kutawala soka na Mourinho akionekana kukwama.

Msimu huu wa EPL tangu mechi ya kwanza dhidi ya Leicester na kipigo kutoka kwa Brighton kumekuwa na mashambulizi mengi kwa Jose Mourinho kutoka kwa mashabiki, wachambuzi na wachezaji wa United wa zamani.

Michezo miwili ya mwanzo ambayo ilionekana mirahisi kwake imeibua mengi, na leo anakutana na mechi ambayo inaonekana ngumu kuliko mbili ambazo wamepitia.

Lakini hii ndio aina ya mechi ambayo Jose anaitaka kwa sasa, hii ndio aina ya mechi ambayo makocha wa kariba yake huwa wanaitumia kuinyamazisha dunia na kinyume cha hapo moto utawaka katika kazi yake.

Tottenham anaenda Old Traford leo wakiwa timu ambayo inaongoza kwa kufungwa katika uwanja wa Old Traford, wameshapigwa mara 21 katika safari zao kwenye uwanja huu.

Lakini Jose Mourinho anaweza kupata tumaini akikumbuka kwamba 1992/1993 ilikuwa mara ya mwisho kwa United kupoteza mara zaidi ya moja katika mechi zao 3 za ufunguzi.

Maurcio Pochettino ni kibonde wa Jose, kwani ameshafungwa mara 11 na Jose Mourinho na Pochettino hajawahi kufungwa na kocha mara nyingi kama alivyofungwa na Mourinho.

Toka mkesha wa mwaka mpya 2014 ambapo Tot waliifunga United, hakuna timu ya London ambayo imeshinda OT, kuanzia siku hiyo timu za London zilichukua alama 7 tu kati ya 66 Old Traford.

Lakini United watachekelea zaidi nkiwakumbusha kwamba katika mechi nne zilizopita kati yao na Tottenham hapa Old Traford, Manchester United walishinda mechi zotee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mourinho anafanya vizuri mechi kubwa leo anaweza akatoa kichapo kwa Totenham
 
Hizi rekodi zinavutia kusoma ila kiuhalisia timu yangu ya Man United kuna kitu hakipo sawa. Hata wachezaji jinsi wanavyocheza unaona kabisa kwamba hawana furaha, hawajitumi kabisa yani. Kama hii timu ingekuwa na morali ya upambanaji uwanjani basi tungekuwa tishio sana hasa msimu huu, maana wachezaji karibu wote wanajuana vizuri sababu wageni ni wachache tu.
SIJUI SHIDA NI KOCHA, ED WOODWARD, WACHEZAJI AU NANI....
GLORY GLORY MAN UNITED
 
Tatizo ni morinho MKUU,,, hana jipya kwa wachezaji KWENYE TIMU PIA,,,na HAKOSI VISINGIZIO KILA KUKICHA..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ManU anakula kichapo heavy
 
kwanini uende mbali huko wakat man u anashinda kiilaini hii gemu? tunaanza na trend ya mechi tano za mwisho ni mwendo wa lose wiin lose win lose win


tunaenda kwenyye head yo head zao wote wanaonekana wababe wanapo kuwa viwanja vya nyumbani
angalia hapa



Hitimisho: sioni sababu ya morinyo kupoteza hii mwchi. Akipoteza basi itakua kwa kutoka droo. Ahsante.

NB kwa wale wazee wa kuweka mikeka kuziacha odds za man u zipotee hivi hivi ni kosa la jinai mahakama ya wanakubet itakukuta na kosa la kujibu.
 
ManU anapigwa.
 
Umeliwa na utabiri wako uchwara angalau kwa sasa!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…