Tottenham Hotspurs Thread

Tottenham imewasilisha ofa ya kumsajili kungo wa kati wa AC Milan Franck Kessie, 24, ijapokuwa haijulikani iwapo Spurs itawasilisha ombi hilo mwezi Januari au kusubiri kumsaini mchezaji huyo wa Ivory Coast katika uhamisho wa bila malipo mwezi January
 
Tottenham Hotspur imefungua mazungumzo na Ajax kuhusu uwezekano ya kumsajili beki wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 20 Jurrien Timber
 
Mshambuliaji wa England Harry Kaane huenda akatia saini mkataba mpya na Tottenham iwapo kifungu cha kumuachilia kuondoka katika kandarasi yake kitawekwa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 awali aliamini kwamba alikuwa na makubaliano ya kiungwana na mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy kuondoka Spurs msimu huu wakati Manchester City ilipojaribu kumsaini.
 
Tottenham na Atletico Madrid wote waliwasilisha ombi la dau la yuro milioni 90 kumsajili mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez ambalo lilikataliwa na klabu ya Inter Milan msimu huu , huku Arsenal pia ikakataliwa baada ya kutoa ofa ya chini.
 
Tottenham inatarajiwa kuwa miongoni mwa klabu zitakazomsajili kiungo wa kati wa klabu ya Calgiari Nahitan Nandez , ambaye pia alikuwa akisakwa na Inter Milan, Napoli, Roma na Fiorentina, wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwezi Januari. Klabu hiyo ya Serie A ipo tayari kumuuza mchezaji huyo mwaka mpya.
 
Huyu mchezaji aondoke akatafute makombe, hapo anapoteza muda.
 
Conte anakwenda kumpiku Ole na kuchukua ile nafasi ya mwisho ya CL.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…