Tottenham Hotspurs Thread

Haya sasa hatimaye mambo yamekuwa mambo. Kama shabiki wa kutupwa wa Spurs ni furaha kubwa kuona Don Levy kaonesha kuwa Spurs ndiyo yapaswa kuwa timu kiongozi pale England.

Baada ya project ya uwanja hatimaye kafanikiwa kufanya project mpya ya squad overhaul bila hata kuhitaji pesa za mafuta au kuvunja kanuni za Fifa Financial Fair Play.

Sasa jana kakamilisha overhaul kwa kununua beki wa kati anayecheza zaidi kushoto kuziba pengo la super Jan Vertonghen. Ndiyo kocha hakupata chaguo lake la kwanza (Milan Skiriniar) ila kapata beki bora wa kati wa Championship League.

Pia inafurahisha kuona genious Levy kaweza kuona umuhimu wa kumpa kocha kile atakacho. Kwako mwalimu Jose kutuletea makombe yote tunayoshiriki.

 
Overhaul imegharimu £70m sawa na gharama ya mchezaji mmoja tu Kai Harvetz wa watani zetu Chelsea [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Hapo ndipo unaweza amini kuwa uchawi upo.

Mwingine naye kanusurika kuibiwa tena mchana kweupe kwa Sancho! Msimu huu burudani kama yote.
 
Tumepata kikosi kipana na kilichoshiba watu wa kazi kazi. Naamini msimu huu hatutatoka patupu
 
Jumla ya gharama za wachezaji wote Levy aliosaini msimu huu unapata gharama ya usajili wa mchezaji mmoja wa Chelsea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…