Tottenham Hotspurs Thread

Loh!
Inabidi kocha usubiri kipenga baada ya dk 90 kipulizwe ndiyo useme nina point 3 mfukon tayari.
 
Hakika leo nimeshuhudia maajabu ya soka. Timu iko nyuma ya mpira dk ya 83 na inaongoza goli tatu. Wachezaji wanaleta utoto na kocha anawapigia makofi ya kuwahamasisha badala ya kuwafokea.

Serge Aurier, D Sanchez, na Winks walikuwa vinara tu, ila kikosi chote ukiacha Kane wamesababisha kupoteza mchezo.

Ngumu kuchukua ubingwa ikiwa tunapoteza points kitoto namna hii.
 
Nimeumia sana leo. Ilibidi tufunge hata goli 5 kwa nafasi tulizopata. Ndombele alikuwa ametawala pale kati alikuwa anahold mipira vizuri kila sehemu ya uwanja yupo, kocha sijui kwanini alimtoa. Ile sub ilivyotokea tu nikalaumu. Sijui kama morali ya wachezaji itaendelea kuwa juu au itashuka tuanze kuchezea vichapo
 
Kikosi ya leo ndiyo hii. Wachezaji wengi muhimu wamepumzishwa.

#COYS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…