Touch, Release, Attack. Kuna watu washaanza kumpigia hesabu kocha wao kumuangushia jumba bovu maana goli moja moja kwa mbinde inawatia wasi wasi!

Makavuli

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2024
Posts
1,425
Reaction score
1,829
Huyu Ramovich ni kama anamchongea kocha mwenzake aliyetumia mechi 15 kufunga goli 31 wakati yeye mgeni katumia mechi 7 na kufunga goli 21. Gusa achia twende kwao imekuwa shubiri upande wa pili maana wanaona kama timu yao inatumia nguvu kubwa kupata ushindi kwa mbinde, wakati wananchi wanatoa kisago cha uhakika!

Wale wameanza kupata wasi wasi mpaka wanafikiria kuukimbia uwanja wa KMC wakidhani wamerogwa🤣🤣 wakati viwango vya wachezaji wao ni vya kawaida sana!

Washaanza kumpigia hesabu kocha wao maana ashaanza kuwapa wasi wasi na ubora wake, zikiwemo mbinu zake, huku ikionekana kabisa ata magoli wanayopata ni aina ya magoli ambayo sio ya mipango uwanjani. Wamekuwa wakinufaika na set pieces ama penalty ama ya offside, lakini sio ya kutengeneza nafasi kwenye open play!

Moto wa Yanga ya Ramovich unawatisha washachungulia na kuona kuna kiama uko mbeleni kinaweza kuwakuta wasipoweka mambo sawa mapema, ikiwemo kuukosa ubingwa kwa mara nyingine tena!

Kuzidi kuimarika kwa Yanga kwa kutoa vichapo mfululizo kuanzia magoli 2+ kunamchongea pakubwa kocha wa timu ya wakina Mutale na Mukwala!

Sasa leo anakwenda kucheza na wabovu wenzake kule Tunisia, unaweza kushangaa akaingia na mabeki 6 tena na bado akagongwa vile vile🤣🤣
 
Hapo umechambua mpira, au umetoa taarabu?
Mahaba tabu sana!
 
IMG-20250105-WA0000.jpg
 
Timu inavimipasho kama Zanzibar modern taarab..kujitafutia umuhimu wakati wala hatuwaoni wa muhimu... 😆 😆 😆 😆
 
Utauonaje umuhimu wakati mgonjwa wako Yuko ICU?
 
Huyu Ramovich ni kama anamchongea kocha mwenzake aliyetumia mechi 15 kufunga goli 31 wakati yeye mgeni katumia mechi 7 na kufunga goli 21. Gusa achia twende kwao imekuwa shubiri upande wa pili maana wanaona kama timu yao inatumia nguvu kubwa kupata ushindi kwa mbinde, wakati wananchi wanatoa kisago cha uhakika!

Wale wameanza kupata wasi wasi mpaka wanafikiria kuukimbia uwanja wa KMC wakidhani wamerogwa🤣🤣 wakati viwango vya wachezaji wao ni vya kawaida sana!

Washaanza kumpigia hesabu kocha wao maana ashaanza kuwapa wasi wasi na ubora wake, zikiwemo mbinu zake, huku ikionekana kabisa ata magoli wanayopata ni aina ya magoli ambayo sio ya mipango uwanjani. Wamekuwa wakinufaika na set pieces ama penalty ama ya offside, lakini sio ya kutengeneza nafasi kwenye open play!

Moto wa Yanga ya Ramovich unawatisha washachungulia na kuona kuna kiama uko mbeleni kinaweza kuwakuta wasipoweka mambo sawa mapema, ikiwemo kuukosa ubingwa kwa mara nyingine tena!

Kuzidi kuimarika kwa Yanga kwa kutoa vichapo mfululizo kuanzia magoli 2+ kunamchongea pakubwa kocha wa timu ya wakina Mutale na Mukwala!

Sasa leo anakwenda kucheza na wabovu wenzake kule Tunisia, unaweza kushangaa akaingia na mabeki 6 tena na bado akagongwa vile vile🤣🤣
Goli moja moja kama hujapoteza mechi nyingi, ni bora kuliko magoli mengi halafu ukapoteza mechi nyingi. Ukitaka kuamini, angalia misimamo ya ligi ya ndani na kimataifa 😂😂😂
 
Sasa wewe msimamo wa ligi unaongoza kwa point ngapi na magoli mangapi tuambie,,
 
Back
Top Bottom