Tovuti gani nzur kwa kuperuz maswali na majibu...hasa kwa ajiri ya assigment?

Vijana wako busy kutafuta VYETI na sio ujuzi.. Ndo kwenye graduation ceremony akitakiwa ku acknowledge waliom support utaskia nashukuru Google,wikipedia, ehow .......

Hahahahahahahahahahahah nimechekaa
 
Dogo suala la maswali na majibu sahau. Naona kama unaulizia 'review' fulani hivi. Kwa kifupi kama hayo mambo yalikusaidia kuvuka Form six uyaache huko huko.

Jibu A mwaka juzi si lazima liwe jibu linalokufaa leo.

Chuo soma intensively kupata mawazo tofauti uweze kupata namna ya kuapproach maswali ya assignment. Huna haja ya kuwa na resource mahususi mtandaoni muhimu ni kusearch kwa uangalifu na tumia zaidi tovuti za vyuo ambazo utazibaini kwa maneno edu.

Pia youtube kuna mambo mengi sana ya msingi kukusaidia. Mule unaweza kukuta lecture za ukweli zilizotolewa katika vyuo maarufu duniani. Video zaweza kukusaidia kutengeneza concept hasa zile ambazo kwa maandishi tu waweza tumia nguvu nyingi kuzielewa na bado usisahau kirahisi. Kwa hivyo ukisearch kwa umakini kwa kutumia keywords nzuri utakuta video zitakazikupanua uelewa wako na hivyo ukafanya assignment zako kwa ufanisi.

Kingine. Penye uwezekano soma zaidi vitabu. Nenda library. Assignment za makundi usiwaachie wenzako we ukaenda kula bata. Itakula kwako. Hakikisha unashiriki kazi kwa asilimia zilizotimia.

Lakini issue ya maswali ya majibu dogo sahau na wala haitakusaidia hata akijitokeza wa kukupa tovuti husika.
 

Wengi tumefaidika na ushauri wenu wakuu binafsi nawashukuru sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…