Tovuti mbalimbali zinazohusu biashara na usafiri

Tovuti mbalimbali zinazohusu biashara na usafiri

Tokyo40

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
2,065
Reaction score
1,925
1. Importer.Tradekey.com
Hapa unauza au kununua vitu tofauti pamoja na matunda na juice kwa jumla.

2. Alibaba.com
Hapa unaweza kuongea moja kwa moja na wenye viwanda
vinavyozalisha vitu tofauti China. Unanunua jumla, bila ya mtu wa kati na kupata bidhaa "customized" kama kiatu au begi lenye logo yako.

3. Agoda.com
Hapa unanunua chumba cha hoteli tofauti duniani kote cha uwezo wako. Ukiwasili nje, huna haja ya kutafuta sehemu ya kulala. Wanakuletea kithibitisho cha ulipaji na booking katika email yako.

4. Booking.com
Tovuti sawa na ya #3 ila unalipa cash ukifika hotelini siyo katika tovuti yao. Hapa unazuia tu chumba kisiuzwe.

5. Orbitz.com
Hapa unaweza kununua chumba cha kulala, ticket ya ndege na kukodisha gari. Unaweza kununua tofauti au kama package (kwa mfano ticket ya ndege dar-lax return, hoteli, gari la kukodisha wiki moja).

6. Travelocity.com
Tovuti sawasawa na #5 .

7. T.justdial.com
Hapa wanauza perfume kwa jumla moja kwa moja kutoka viwandani huko India.

8. Tripadvisor.com
Lonelyplanet.com
Fodors.com
Forum.virtualtourist.com
Kwenye hizi tovuti unaweza kujitangazia hoteli yako, kujibu maswali ya watalii mbalimbali, kusoma hoduma za hoteli mbalimbali kutoka kwa wageni (reviews) na kutafuta mtalii.

9. Ofisi za Ubalozi mbalimbali.
Ubalozi wa nchi nyingi wana afisa anayeshughulikia biashara (commercial attaché).
Anaweza kukupa contact za wafanyabiashara tofauti wa kwao na kujibu maswala mengi kuhusu sheria zao na jinsi ya kujaza fomu zao unapotaka kusafirisha bidhaa.

10. Bestvaluewineguide.com
Hapa unaweza kununua mvinyo wa Afrika Kusini kuanzia US$2 kwa chupa.

11. Startups.co.uk
Sehemu ya kutafuta wanunuzi wa vikapu, bangili na vitu vingine vya kiasili vinavyotengenezwa na mkono
(Handmade African Crafts). Wafanyabiashara wa vitu hivi wanakusanyika hapo.

12. cic.gc.ca
Tovuti ya serikali ya Kanada. Inakuonyesha jinsi ya kujipatia viza ya kuhamia kwao (permanent immigration visa) kwa kutumia elimu/fani yako.

13. Australia.gov.au
Tovuti kama ya #12 lakini kwa ajili ya Australia.

14. ebay.com
Hapa ni mnadani. Uza na kununua unachokipenda.

15. Tradecarview.com
Unaweza kununua magari yaliyotumiwa kutoka Japan hapa.

16. Tradeindia.com
Tafuta bidhaa unayotaka. Pata contact ya mwenye kiwanda kinachotengeneza bidhaa hiyo huko India.

17. Thecoffeelocator.com
Jiunge katika tovuti hii ili uweze kuuza kahawa yako moja kwa moja kutumia tovuti yao kwa mnunuzi badala ya kutumia mtu wa kati.

18. Bigsite.jp/english/
Wasiliana na wahusika wa Tokyo Big Site, Japan hapa ili uweze kuhudhuria maonyesho ya biashara inayokuhusu.
Ni kama uwanja wa "Saba-Saba". Kwenye maonyesho ya utalii, utakuta nchi 100 au zaidi zinahudhuria kuwavuta watalii watembelee kwao.

19. Yelp.com
Kama unataka kwenda hospitali au sehemu za starehe au kula chakula cha nchi fulani miji ya watu, njoo hapa. Andika mji na nini unahitaji. Inakupa jina, ramani na anuani. Haina miji yote.

20. Hyperdia.com
Hii tovuti ya Kiingereza itakuonyesha njia, mda wa usafiri, kituo cha kubadili treni (ikihitajika) na bei za usafiri wa treni nchini Japan. Andika jina la kituo ulipo na jina la kituo unachokitaka kwenda.

21. Scholarships.com
Ni tovuti ya kutafuta mdhamini katika vyuo mbalimbali vya Marekani.

22. University of Edinburgh, UK
The Julius Nyerere Master's
Scholarship (ad.ac.uk)
Mtanzania aliyesomea Tanzania tu, anaweza kupata udhamini wa mwaka mmoja katika somo lolote (Master's).
Omba mapema. Ombi la 2015-2016 limeshafungwa.

23. Touropia.com
Jua vivutio kumi bora vya kitalii vya Uturuki.

24. goturkey.com
Tovuti ya kitalii kama ya #23 lakini ya serikali ya Uturuki. Ina habari zaidi.

25. evisa.gov.tr
Maombi ya viza ya miezi 6 ya Uturuki kwa njia ya elektroniki hupokelewa hapa kwa raia wa nchi mbalimbali.

26. Tourismthailand.org
Tovuti ya habari za kitalii ya serikali ya Thailand.

27. Spain-property.com
Nunua nyumba hapa, utapewa visa ya kuishi Spain wewe na familia yako na njia ya kupata uraia wao ukipenda. Mtaji: Euro 500,000.

28. ccmalta.com
Tovuti ya kuonyesha jinsi ya kupata viza ya kuishi Malta (EU) kwa kununua nyumba.
Mtaji: Euro 220,000.

29. Africaimports.com
Wanauza bidhaa mbalimbali kutoka Afrika katika mtandao. Wasiliana nao kama una bidhaa ya kuuza au kununua. Wapo NJ, USA.

30. talkenglish.com
Tovuti bure ya kujifunza Kiingereza.

31. learnamericanenglishonline.com
Tovuti bure ya kujifunza Kiingereza cha Kimarekani.

32. oedb.org
Tovuti hili lina masomo mbalimbali unayoweza kusoma bure ukijiunga nao. Pata elimu ya bure kutoka kwa walimu wa vyuo mbalimbali vya Marekani kwa kupitia mtandao.

33. edx.org
Tovuti ya elimu ya bure kwa njia ya mtandao. Sawa na #32 .

34. Importers.com
Tovuti hii inawakutanisha wanunuzi na wauzaji wa jumla wa bidhaa mbalimbali kutoka nchi mbalimbali. Ina wanachama 350,000.

35. useximafricaevents.com
Ijue AGOA vizuri kwa hudhuria mkutano wa pili wa biashara kati ya bara la Afrika na Marekani.
Baltimore, Maryland, USA. September 8-9, 2015.

36. skyscanner.com
Tovuti hii inakutafutia bei za usafiri wa ndege zilizotangazwa katika tovuti mbalimbali za usafiri kwa pamoja.

37. thesitewizard.com
Tovuti hii inakufundisha jinsi ya kuanzisha tovuti yako ya kuuza bidhaa katika mtandao.

38. investinginafrica.net
Tovuti la habari zinazohusu manunuzi ya hisa Afrika. Kuna habari ya kufundisha namna ya kuuza na kununua hisa Tanzania (TSE).

39. guides.wsj.com
Tovuti la gazeti maruufu la kibiashara la Marekani. Soma muongozo hapa wa namna ya kununua na kuuza hisa Marekani.

40. indeed.com
monster.com
jobsDB.com
Tovuti za kutafuta kazi mbalimbali nchi za nje.

41. idealist.org
Tovuti ya kutafuta kazi mbalimbali za mashirika ya "non-profit" (Tanzania na nje).

42. careers.un.org
Tovuti ya kutafuta kazi mbalimbali za Umoja wa Mataifa.

43. japanusedbicycles.com
Agiza baiskeli zilizotumika kutoka Japan katika tovuti hii.

44. aisha.co.jp
Agiza hapa baiskeli, pikipiki, mabasi, magari na spea za magari zilizotumika kwa bei ya jumla kutoka Japan.

45. globalsources.com
Wasiliana moja kwa moja na wazalishaji wa bidhaa tofauti za jikoni kutoka China.

46. jovago.com
Tafuta chumba cha kulala katika tovuti hii ya hoteli katika miji mbalimbali duniani.

47. bamboulaltd.com
Tovuti la muuzaji wa vikapu na vitu vingine vilivyotengenezwa na mkono kutoka Tanzania/Afrika. Yupo USA.

48. fordaq.com
Tovuti za contact za waagizaji wa mbao mbalimbali wa UAE.
 
asante sana mkuu yaani umetusaidia wengi
maana mm ninasafari nov huyo turkey na thailand
 
Back
Top Bottom