Tovuti za Serikali hazina ufanisi kabisa

Tovuti za Serikali hazina ufanisi kabisa

P J O

Senior Member
Joined
May 3, 2024
Posts
189
Reaction score
264
Habari za Asubuhi. Twende Moja Kwa Moja kwenye mada.

Serikali kipindi Cha JPM na Kikwete waliwekeza sana kwenye kuboresha mifumo ya TEHAMA, foleni kwenye maofisi ya serikali, Hospitalini zilipungua kiasi kikubwa lakini Bado Kuna changamoto kwenye kuomba maombi kwenye tovuti zao, Tena changamoto kubwa.

RITA, ukishatengeneza account, ulitaka kusign in wanakuomba username wakati username hawajakupa, no customer care . 😐

TRA, mifumo ya kupata TIN number kila leo inacollapse na hawatoi taarifa.

Tovuti za kutuma maomba ya vyuo vya serikali kama Muhimbili ndio usiseme. Hapafai kabisa.

Nisiendelee mwenyewe, Taja tovuti nyingine za serikali ambazo ulitoka povu kupata huduma
 
Na Kila Leo wanaajiri watu wa tehama na kulipwa mshahara na posho Kila siku. Ukihujumu/ kuharibu vya umma system itakusafisha yenyewe kama bahari inavyosafisha yenyewe takataka zote kuziweka mbali pwani.

Nikama juzi tunaambiwa watumishi wa umma wenye tallents na gifts hawatumiwi wanawekwa pembeni huku wakilipwa Bure .
 
😅😅😅 tuna safari ndeefu sana!! Sio kwamba watu hawawezi kuweka ya kueleweka!! Ni kwasababu wanahisi wanafanya Bure hawalipwi
 
Hayo mataka taka kero Sana.
Na kale katabia kao Mtandao uko chini kila siku.
 
Hata mfumo wa TRA kwa ajili ya kuomba zile Nafasi za kazi, mpaka Sasa ni hola vijana wanashindwa kutuma maombi..
 
Back
Top Bottom