Haya majina huwa wanabadili kutokana na Soko. Waweza kuta gari hiyohiyo kwa Soko la japan ikauzwa kwa jina X alafu soko la Asia ikauzwa kwa jina Y na Marekani ikaitwa Z nk nk.
Hio inatokea kwa gari nyingi tu, sasa katika kubadili majina sio lazima zifanane kila kitu, zinaweza fanana muonekano lakini zisifanane specification au zikatofautiana tu wheel base au bamper, au moja ikanyanyuliwa kidogo au ikawa modified ndani kupata space nk nk yapo mengi sana mengine ni ya kuangalia kwa jicho lanl kitaalam
Sasa Allex na RunX kuna kihistoria chake mpk zikabadilishana majina ila zikiwa zinafanana kama alivosema mdau hapo moja ni kwa soko la japane nyingine nje ya japane lakin katika kuzifuatilia sana utagundua kiufundi Allex iliboreshwa kidogo ili kuongezwa confortability kwa watu wazima Alafu RunX ikaachwa ina sound sana kwaajili ya vijana hata kukimbia kiufundi RunX inamzunguko mkubwa kuliko Allex kwa maelezo zaidi pitia Wikipedia