Toyota brevis vs toyota mark x

rajabkisauti

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2015
Posts
566
Reaction score
316
Nataka ninunue gari moja tajwa hapo mwezi wa ujao mungu akipenda.
Naombeni ushauri kuhusu hizo gari ipi ninunue..
NB:sihitaji gari aina nyengine zaidi ya hizo tajwa hapo juu.
WATAALAM NISAIDIENI KWENYE UCHAGUZI WA GARI[emoji41]
 
Chukua mark x, ila kama unakaa uswahili itakusumbua maana ipo chini sana
 
Nataka ninunue gari moja tajwa hapo mwezi wa ujao mungu akipenda.
Naombeni ushauri kuhusu hizo gari ipi ninunue..
NB:sihitaji gari aina nyengine zaidi ya hizo tajwa hapo juu.
WATAALAM NISAIDIENI KWENYE UCHAGUZI WA GARI[emoji41]
Kwa sifa, almost zote ziko sawa ila mark x ni bora zaidi kwa perfomance zaidi ya brevis na ndio maana hadi leo bado inatengenezwa!

Japo brevis sio mbaya, nayo ni nzuri pia, ila kwenye perfomance mark x ndio iko vizuri zaidi.

Na hata kimuonekano na hadhi, mark x ni nzuri zaidi ya brevis.

Ulaji wa mafuta inategemeana sana na maeneo ulipo pamoja na mwendo wako!

Hata spare upatikanaji wake ni mwingi sana ...

Huo ndio ushauri wangu kwako nikiwa kama muuzaji magari!

Ukiwa tayari, unaweza kunipa Mimi hio order, nikakuletea from japan kwa bei chee kabisa.

Unaweza kupitia hapa, kuona baadhi tu ya gari ninazo uza ...

Kwa mnaohitaji kununua magari - tukutane hapa
 
Nenda Mark X kama unakaa mjini. Kama unakaa kwenye makorongo sana nenda Brevis. Mark X laini sana.
 
Mkuu, nataka harrier hybrid, naomba unipe specification zake na gharama
 
Sawa Mkuu pamoja tutatafutana
 
Mark x gari..za kirembo izo...chukua mnyama brevis kokote twende tu..
 
Ulaji wa mafuta ipi afadhali katika brevis na mark x >2007
Kwanza hongera sana kwa kuwa na uwezo wa kununua gari haswa wakati huu wa uchumi wa mwendokasi. Nimesoma ushauri wa watu wengi humu nafikiri wengi wapo sawa kabisa. Brevis ni platform ya zamani na walishaacha kuzitengeneza kwa hiyo ni bora uende na mark x. Na kwa kuwa Mark X zilianza tengenezwa 2004,huwa ni vizuri kutonunua model ya mwaka wa kwanza maana huwa hakuna feedback. Kwa hiyo watengeneza magari huwa wanarekebisha sehemu ambazo zimelalamikiwa zilizopo kwenye model ya mwaka wa kwanza. Kwa hiyo ni vizuri sana ukanunua za kuanzia nafikri 2007 na kuendelea.
Kwa ulaji wa mafuta sijafanya uchunguzi wa kina ila tu nitaenda na uzoefu hapo.
Tuanze na upande wa engine za Brevis ambayo inatumia inline 6(Six cylinders flat configuration) na ni 2500 cc to 3000cc.
Mark X wametumia V6 configuration na displacement ni 2500cc to 3000cc.
Tukichukua kwa mfano entry level engine ya Brevis vs Mark X ambayo in 2500cc,unapata 210 HP na torque ni kama 190LB wakati kwa Brevis utapata 190hp na torque ni 180LB.
Sasa kwa mpango huo basi inaonesha kuwa engine za Mark X zipo more efficient compared to old generation inline six used in Brevis,kwa mpango huo,utapata better fuel consumption kwa Mark X.
Pia zingatia upatikanaji wa vipuri,kwa gari ambazo hazitengezwi tena,kadiri siku zinavyopita ndo vipuri vinakuwa tabu kidogo.
Mwenye la ziada ataongezea hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…